Saturday, 2 January 2016

UCHAMBUZI WANGU KUHUSU MAKOCHA WA KIGENI NA WAZAWA

benado kikoti mwandishi wa mtandao wa HABARIKA TZ

  Kuwepo kwa  makocha wa kigeni hapa nchini limekuwa ni suala lakawaida sana tujiulize maswali kwani wazawa hawawezi kufundisha ambatana nami wa uchambuzui zaidi

Msomaji wangu tuanze kuiangalia timu ya taifa ambayo imekuwa ikinolewa na makocha wa kizungu katika vipindi tofauti tofauti kama Marcio Maximo, Paulsen, Mart Nooij na wengine kwa kutaja hao wachache tu.

Pia siyo timu ya taifa tu vilabu navyo vimekuwa vikiwaajiri makocha wa kigeni .Hawa ni makocha waliwahi kuinoa Yanga SC: Sam Timbe (Uganda), Kostadin Papic (Serbia), Tom Saint Fiet (Ubelgiji), Ernest Brandts (Uholanzi) Marcio Maximo (Brazil) hao ni makocha wacheche waliowahi kuinoa Yanga, na sasa ni Hans van der Pluijm ambaye ni Mholanzi.
Lakini simba nao wamekuwa na makocha kama Patrick Phiri (Zambia), Milovan Cirkovic (Serbia), Mosses Basena (Uganda), Patrick Liewig (Ufaransa), Zdravko Logarusic (Croatia), Goran Kopunovic (Serbia) na sasa Dylan Kerr ambaye ni Muingereza.

Mfano mzuri ni kwa kocha bonface mkwasa ambaye ni kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa stars tangu akabidhiwe kikosi unaona kabisa kuna mwanga ambao wachezaji wanapata hatuna haja ya kukalili kuwa wazawa hawawezi.

Bila shaka umejifunza kitu kutokana na hilo ndiyo maana kocha wa mwadui fc ya shinyanga yeye amekuwa akisema wazawa hawapewi tu nafasi lakini wanaweza na siyo hivyo tu pia suala la wachezaji nalo amekuwa akilipigia kelelea sana kuwa wachezaji wa nje wiwango vyao ni sawa na wachezaji wa ndani

No comments:

Post a Comment