![Watford](https://i.guim.co.uk/img/media/58278669c5713a77ea0c596ec7c5096a1b29c0e6/0_156_4974_2985/master/4974.jpg?w=300&q=85&auto=format&sharp=10&s=4eb28e7a5deef9f1f245c8e2780d4969)
MENEJA wa Watford, Quique Sánchez Flores na Mchezaji wake, Odion Ighalo, ndio wametunukiwa Tuzo za Meneja Bora na Mchezaji Bora za Ligi Kuu England kwa Mwezi Desemba zinazotolewa na Wadhamini wa Ligi hiyo, Barclays.
Kikosi cha Flores kilizoa Pointi 10 katika Mechi zao 5 za Mwezi Novemba kwa kuzifunga Norwich, Sunderland na Liverpool na kutoka Sare na Chelsea na kupanda kuwa kwenye Timu 10 za juu kwenye Msimamo wa Ligi.
Flores, anaetoka Spain, amewabwaga Arsène Wenger, Claudio Ranieri na Alan Pardew kwa kutwaa Tuzo hii.
Nae Ighalo, Mchezaji kutoka Nigeria aliefunga Bao 5 Mwezi Desemba, amewabwaga Mesut Özil, Marko Arnautovic, Riyad Mahrez, Romelu Lukaku na Dele Alli, na kushinda Tuzo ya Mchezaji Bora.
Mechi inayofuata kwa Watford ni ya Ugenini dhidi ya Swansea City.
LIGI KUU ENGLAND
Jumamosi Januari 16
1545 Tottenham v Sunderland
1800 Bournemouth v Norwich
1800 Chelsea v Everton
1800 Man City v Crystal Palace
1800 Newcastle v West Ham
1800 Southampton v West Brom
2030 Aston Villa v Leicester
Jumapili Januari 17
1705 Liverpool v Man United
1915 Stoke v Arsenal
Jumatatu Januari 18
2300 Swansea v Watford
No comments:
Post a Comment