Mwanasheria
Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu
ameeleza kuwa tayari majibu ya maswali yaliyoulizwa kuhusu Edward
Lowassa kuwa mali au mzigo kwenye chama hicho yamejidhihirisha wazi.
Swali
hilo liliulizwa na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama hicho, Dk. Wilbroad
Slaa aliyedai kuwa alishindwa kupata majibu kama ujio wa Lowassa kama
anaingia kwenye chama hicho kama mzigo au mali.
Akizungumza
na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki iliyopita, Tundu Lissu
alieleza kuwa tayari majibu hayo yako wazi kuwa Lowassa ameweza kuvipa
vyama vinavyounda Ukawa uwezo wa kushika Halmashauri za jiji la Dar es
Salaam hatua ambayo haijawahi kufikiwa na chama chochote cha upinzani
tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi nchini. Hivyo, ni mali na sio
mzigo.
“Tangu upinzani uingie ncbini haujawahi kuishika Dar, Lowassa ameiteka Dar,” alisema Lissu.
Uchaguzi
wa Umeya uliofanyika wikendi iliyopita uliwezesha diwani wa kata ya
Ubungo kwa tiketi ya Chadema, Boniface Jackob kushinda nafasi ya umeya
wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, huku nafasi ya Naibu Meya
ikienda kwa Jumanne Mbulu wa Chama cha Wananchi CUF.
Kwa
upande wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Nafasi ya Umeya ilishikwa
na Charles Kayeko wa Chadema na naibu wake ni Omari Kumbilamoto wa CUF.
Vyama
vinavyounda Ukawa pia vimeweza kushika Halmashauri za majiji ya Arusha,
Mbeya na Halmashauri nyingine za miji na manispaa ambazo zilikuwa
mikononi mwa CCM.
No comments:
Post a Comment