Mwanasheria wa aliyekuwa Rais wa
shirikisho la Soka Duniani FIFA Sepp Blatter anatarajiwa kuwasilisha
rufaa yake kupinga kufungiwa miaka minane kujishughulisha na masuala ya
soka.
Hata hivyo kamati ya nidhamu ya FIFA imewasilisha sababu za
kuchukuliwa kwa hatua za nidhamu dhidi ya viongozi hao waandamizi wa
zamani wa soka Blatter na mwenzake, Michel Platini. Mwezi Disemba
aliyekuwa Rais wa FIFA Sepp Blatter na rais wa UEFA Michel Platini
walifungia kwa kipindi cha miaka minane baada ya kukutwa na hatia ya
kuvunja kanuni na sharia za FIFA. Kwa upande wake pia mwanasheria wa
Platini anasema kuwa anatarajia kukata rufaa kwa kupinga maamuzi ya
FIFA. CHANZO BBC
No comments:
Post a Comment