Ripoti kutoka nchini Iraq zinasema
kuwa familia zilizopo kaskazini mwa mji wa Hawijah zinayahama makazi yao
kuhofia njaa na utawala wa kundi la wapiganaji wa Kiislam IS.
Shirika
moja la habari la Ufaransa limesema kuwa kumekuwa na vifo vya raia
ambao wanalazimika kutembea umbali mrefu milimani ili kuweza kuyafikia
maeneo salama nchini Iraq. Mwanamke mmoja amesema kuwa mabomu
yanayowakumba njiani,yamesababisha kifo cha mume wake na mtoto wake wa
kiume wakati wakijaribu kulihama eneo hilo. Hawijah ni ngombe ya
wapiganaji wa Islamic State,lakini makundi ya wapiganaji wa Kikurdi
wanadaiwa kudhoofisha nguvu ya kundi hilo
No comments:
Post a Comment