Mawaziri wa ulinzi
wa nchi za magharibi wanaokutana jijini Paris wamekubaliana kuongezea
nguvu zaidi kampeni dhidi ya wanamgambo wa Islamic State nchini Iraq na
Syria.
Waziri wa ulinzi wa Marekani, Ash Carter amesema wana nia kuu tatu ambazo ni kuisambaratisha IS katika ngome zake za Raqqa na Mosul, kupambana na matawi yake duniani kote na kulinda raia.
Mawaziri wa ulinzi kutoka nchi 27 zikiwemo Iraq na nchi kadhaa za kiarabu watakutana mjini Brussels mwezi ujao.
No comments:
Post a Comment