Sauti yake pia ni nzito.
Huyu ni Mirr Abdullahi, mwanamume mwenye umri wa miaka 40 aliyekimbia mapigano Somalia miaka kumi iliyopita.
Amemwambia mwandishi wa BBC Bashkas Jugsodaay kwamba changamoto kuu anayokumbana nayo kambini ni kwamba watu humfanyia mzaha. Watoto pia humfuata kila aendako.
Kutokana na upweke, yeye hutumia muda wake mwingi akitafuna miraa na kuvuta sigara.
Pesa hupata kutoka kwa wahisani kambini.
Anasema akirudi huko, ana wasiwasi kwamba hali ikiwa mbaya hawezi kukimbia na kutoroka kama watu wengine.
No comments:
Post a Comment