Saturday, 9 January 2016
MESSI, HETITRIKI, NEYMAR, WAIRUDISHI BARCA KILELENI LA LIGA
NDANI ya Nou Camp, mbele ya Mashabiki 70,720, Barcelona iliinyuka Granada Bao 4-0 kwa Bao 3 za Lionel Messi na 1 la Neymar, na kuchukua uongozi wa La Liga.
Hadi Mapumziko Barca walikuwa mbele 2-0 kwa Bao za Dakika za 8 na 14 za Messi ambae Kipindi cha Pili alipiga Bao la 3 Dakika ya 58. Na Neymar kupiga la 4 Dakika ya 83.
Ushindi huu, ambao ni Mechi ya kiporo, umewaweka Barca kileleni wakiwa Pointi 1 mbele ya Atletico Madrid na Pointi 5 mbele ya Real huku zote zikicheza Mechi 18
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment