Saturday, 9 January 2016

Makosa makubwa 10 wanaume wengi hufanya wakiwa faragha

Image result for MAHUSIANO

Ukitaka kujua uhondo wa ngoma sharti uingie ndani ucheze si ndio, kuna mambo ya kuwahusu wanaume huwezi yasikia kwa wanaume wenyewe lakini ukikaa na wanawake wanaweza kukwambia ni makosa gani wanaume wanayafanya hasa wakiwa faragha,ambayo hayawapendezi na wanaume wengi huwa hawajui kama hayo ni makosa .
Kuandaa Mazingira
Mazingira, naongelea muonekano mzima, wa eneo la tukio lazima kuwe kusafi, sio nguo chafu ziko kila sehemu, sebuleni umeweka makopo ya soda yameisha vipande vya mkate, viatu vya matope ilimradi shida, lakini wengi wanashindwa kuandaa mazingira, weka nyumba yako safi, manukato, mziki mzuri weka mwanga mdogo au la washa mishumaa,kuweka mazingira yavutie kabla ya game.
Maandalizi
Kwa mwanamke yeyote, maandalizi ya mwanzo kabla ya show nzima ni muhimu sana, ila wanaume wengi wanaharaka ya kumaliza mchezo, hata wachezaji mpira wanafanya kwanza warm up kabla ya kuingia uwanjani unadhani kwanini? Kwahiyo cha muhimu ni kukumbuka jinsi ya kumpa mwenza wako maandalizi ya kutosha yanahitajika sana.
Kuwa na Papara
Kuna watu wana papara, unashindwa kufanya maandalizi ya awali na bado unaharaka kama mwana riadha, sio adhabu wala sio ugomvi wanawake wanapenda kulelewa, nenda nae taratibu muachie muda wa kupumua, sikiliza mapigo yake ya moyo, muongeleshe taratibu, alafu uendelee .
Kutokujua Kusoma Mchezo
Wanawake wengi wana aibu ya kusema nini wanataka wakiwa kitandani, ila kuwa mjanja na usome alama za nyakati wanaume wengi wanafeli hapo, kuna wakati wa kuongea kama mabubu, ni wewe tu kujua nini maana yake,usisubiri uambiwe, kwahiyo kuna wakati unashindwa kumpa mpenzi wako huduma anayoitaka sababu hukuweza kumsoma nini anataka.
Unataka kufanya vitu vingi kwa wakati mmoja
Sio kila staili uliyoiona unataka kugeza siku moja, kuwa mstaarabu na jaribu kila moja kwa wakati, haina haya ya kufanya zote kwa siku moja, na mambo mengine pia sio ya kugeza, mnaweza kuongea kabla ya kuanza kitu kipya kama na mwenza wako yupo tayari kwa hilo, usilazimishe. Ingependeza kama mtafanya vitu kila mtu anafurahia na mtakuwa huru kufanya mambo yenu kwa amani.
Kumvunjia heshima mwenza wako
Kuna baadhi ya vitu si  kila mwanamke anapenda kufanyiwa,kama kumuita majina ya ajabu ajabu uliyo ona katika filamu Fulani au video za ngono, usifanye mambo hayo wengine hawajisikii vizuri kufananishwa na wale wanawake wa kwenye video za ngono, baadhi ya wanawake huchukulia swala hili kama kumvunjia heshima, na  wapo wanaume wanafanya michezo hii. Kitu ambacho kiukweli  hakipendezi.
Usijifanye Wewe ndio Kiongozi
Wapo wanaume wanapenda kuwa viongozi kila sehemu lakini sio kitandani bwana, mnatakiwa kuwa na ushirikiano,sio kila kitu unataka kwa kulazimisha, kuwa mtaratibu na mstaarabu na unaweza ukamuacha  mpenzi wako afanye anachotaka kufanya na wewe bila wewe kutoa maelekezo.
Kusahau Sehemu Muhimu
Kila mtu ana sehemu za kumfanya apate mzuka zaidi wapo wanaume wanasahau haya, wao wanajua kuwahi tu sehemu wanayoitaka wakiwa kitandani ni kosa, jua kucheza na mwili wa mwenza wako,lazima ujue ni wapi mpenzi wako anapenda kushikwa ama kutomaswa wakati wa faragha
Kuhisi Karidhika
Usijidai kwamba wewe unajua kutoa show kali basi lazima atakuwa amefurahia, muulize kama ameridhika, wanaume wengi hawaulizi ili, ni kosa unaweza ukawa hata hujampa kile alichokuwa anataka  na kwa sababu wanawake wengi sio watu wa kuweka mambo wazi  hatoweza kukueleza kuhusu alivyojisikia. Ila anaweza sema kama ukiuliza.
Kumfanya kiburudisho
Kuna baadhi ya wanaume wanawafanya wanawake zao  kama kiburudisho akimaliza haja zake anavaa na kuondoka, au ndo akimaliza atageukia upande wa pili na usingizi juu, tafadhari sio mchezo mzuri kufanya hayo kwa mwenza wako, inapendeza kama mtaongea hata kwa nusu saa  baada ya kumaliza kabla ya kila mtu kufanya yake.

No comments:

Post a Comment