Saturday, 2 January 2016

Kardinali Pengo alazwa Muhimbili

ASKOFU Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo amelazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete iliyopo Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam. Pengo alifikishwa katika katika Taasisi hiyo Desemba 31, mwaka jana jioni kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa afya yake. Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa ilisema Rais John Magufuli akiongozana na mkewe, Mama Janeth walimtembelea Pengo na kumjulia hali.
Magufuli alimpa pole Askofu Pengo na kumuombea afya njema ili aweze kuendelea na shughuli zake za kutoa huduma za kiroho kwa wananchi. Mkurugenzi wa Taasisi hiyo ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Profesa Mohamed Janabi, alisema hali ya Kardinali Pengo inaendelea kuimarika, ikilinganishwa na alipofikishwa katika taasisi hiyo

No comments:

Post a Comment