Droo ya kupanga Mechi za Raundi ya 4 ya EMIRATES FA CUP imefanyika Usiku huu bila kuibua zile Bigi Mechi.
Mabingwa Watetezi, Arsenal, wao watakuwa Nyumbani kwao Emirates kucheza na Timu ya Daraja la chini Burnley wakati Mabingwa wa Ligi Kuu England, Chelsea, wakiwa Ugenini kucheza na Mshindi kati ya Northampton Town au MK Dons.
Man United wao wako Ugenini kucheza na Timu ya Daraja la chini Derby County na vile vile Man City wako Ugenini kupambana na Mshindi kati ya Wycombe Wanderers au Aston Villa.
Liverpool, ambao walitoka Sare na Exeter City katika Raundi ya 3, wakishinda Mechi yao ya Marudiano itakayochezwa kwao Anfield, watabaki hapo hapo kwao kuikwaa West Ham.
Mechi hizi za Raundi ya 4 zitachezwa Wikiendi ya Ijumaa Januari 29 hadi Jumatatu Februari 1.
DROO KAMILI:
West Brom au Bristol City v Peterborough United
Eastleigh au Bolton v Leeds United
Arsenal v Burnley
Derby County v Manchester United
Huddersfield Town au Reading v Walsall
Exeter City au Liverpool v West Ham
Wycombe Wanderers au Aston Villa v Manchester City
Shrewsbury Town v Sheffield Wednesday
Nottingham Forest v Watford
Carlisle United au Yeovil v Everton
Crystal Palace v Stoke City
Oxford United v Newport County au Blackburn Rovers
Ipswich Town au Portsmouth v Bournemouth
Colchester United v Tottenham au Leicester City
Bury au Bradford City v Hull City
Northampton Town au MK Dons v Chelsea
THE EMIRATES FA CUP 2015/16
TAREHE MUHIMU
Raundi ya 3
Ijumaa 9 Januari 2016
Raundi ya 4
Jumamosi 30 Januari 2016
Raundi ya 5
Jumamosi 20 Februari 2016
Raundi ya 6-Robo Fainali
Jumamosi 12 Machi 2016
Nusu Fainali
Jumamosi 23 Aprili 2016 & Jumapili 24 Aprili 2016
Fainali
Jumamosi 21 Mei 2016
No comments:
Post a Comment