Rais Barack Obama
wa Marekani amekubali kutoweka bayana mipango ya serikali yake katika
mapambano dhidi ya ugaidi duniani na hasa kundi la wanamgambo wa dola
ya kiislam maarufu kama Islamic State.
Rais Obama alitoa tamko hilo katika mahojiano ya wazi yaliyofanywa mwanzoni mwa wiki hii akiwa mapumzikoni nje ya nchi yake; yeye na familia yake katika visiwa vya Hawaii.
Rais Obama hakusita kuelekeza shutuma zake kwa mgombea wa chama cha Republican anayegombea nafasi ya urais, Donald Trump kwa kuleta mkanganyiko pamoja na kuzidisha wasiwasi na kuwataka wanaume waliostaarabika na wenye elimu ya kutosha kuongeza nguvu katika kampeni za mgombea huyo.
Trump aliwahi kutoa wito wa kuzuiliwa waisilamu kuingia nchini Marekani baada ya shambulio la hadhara mjini California lililosababishwa na wapenzi wawili wanaoaminika kuwa ni watu waliokuwa na msimamo mkali.
No comments:
Post a Comment