Wednesday, 30 December 2015

Njia 5 za kupata mafanikio


Katika makala zangu zilizopita niliwahi kuandika kuhusu  ‘’Mbinu za kukusogeza karibu na mafanikio


1. Kuwa na malengo/mtazamo chanya wa ndoto zako za kufanikiwa kimaisha.

Washindi hupata wanachohitaji kwasababu wanajua nini wanataka. Wana mitazamo chanya ambayo inawahamasisha na kuwapa nguvu kufikia malengo yao. Ni sawa na kutaka kufika mahali fulani, ili uweze kufika utakapo ni lazima uwe na lengo. Jiwekee malengo leo na anza kufuata ndoto zako.

Soma pia:  Mbinu 5 za kuwa mstahimilivu katika kuyaendea malengo yako

2. Kuwa na shauku ya kutaka kufanikiwa.

Kiu ya mafanikio ni kichocheo cha kuyaendea malengo yako mpaka ufikie juu ya kilele cha mafanikio. Utafutaji wa mafanikio unahitaji nia ama kiu isiyokwisha uwapo safarini kuelekea unapokusudia.

3. Ishi kwa ukweli.

Ukweli ni moja kati ya njia zinazoweza kukufanikishia malengo yako. Kuwa mkweli kwako mwenyewe, huwezi kufanikiwa ilhali unajijua ni mvivu, mzembe, huna bidii au huwajibiki na maisha yako. Mfano unataka kuwa na pesa lakini hujishughulishi kuzitafuta. 

Ni vyema ukatambua uhalisia wa maisha yako uko vipi kabla ya kufikiria kufanikiwa mambo makubwa. Usijidanganye kwa kuwa na ndoto za abunuwasi, unayo kila sababu ya kubadilisha sura na muelekeo wa maisha yako. Ikiwa hujaridhika na maisha uliyonayo sasa huu ni ndio wakati wa kubadilika kwa kuanza kutafuta maisha mazuri utakayo. 

4. Kubali mabadiliko.

Kuwa mwepesi kubadilika, mara nyingi njia za mafanikio hutofautiana kwa mtu na mtu licha ya kuwa kuna zile tabia za mafanikio ambazo ni lazima kila mtu awe nazo. Usiwe mtu mwenye mawazo mgando, badilika kulingana na ukweli wa mambo unavyokutaka nini ufanye ili ufanikiwe. 

Mabadiliko ya kimaisha (uchumi, ushirikiano na mahusiano baina ya watu, upatikanaji na utendaji wa kazi) vyote hivi vinakuhitaji ubadilike kulingana na mambo yalivyo. Kuwa tayari kuendana na mabadiliko yanayotokea kila siku.



5. Kuwa tayari kupambana na changamoto.

Katika kutafuta mafanikio utakutana na changamoto nyingi hivyo kuwa tayari kwa lolote litakalotokea. Kuwa tayari kukutana na vizuizi ambavyo vitakuhitaji usimame imara. 

Watu, pesa na vitu vingine vyote ambavyo kwa namna moja au nyingine vitakuwa changamoto kwako ni vyema utilie nidhamu ya juu katika utatuzi ili usonge mbele kwa uhakika. Mbinu na njia sahihi utakazopitia kuyaendea malengo yako ndizo zitakazokufikisha mahali utakapo.

6. Jenga mahusiano mazuri na watu ambao tayari wanamafanikio.

Jifunze kwa watu ambao tayari wanamafanikio kama hayo unayokusudia kufanikiwa. Dadisi mambo mengi kutoka kwao, wasome na kuwajua vizuri ili uweze kufikia malengo yako. Kwa kutumia siri zao za mafanikio (fikra, mbinu, mikakati n.k) utaweza kufika mbali kimaendeleo.

No comments:

Post a Comment