alie kuwa mgombea mwenza kupitia chama cha CHADEMA katika uchaguzi muu wa mwaka 2015 Juma Duni Haji amesema hatima yake ya kubakia au kuondoka ndani ya Chadema itajulikana mwezi ujao.
Duni
aliihama CUF na kujiunga Chadema ambayo ilimsimamisha kuwa mgombea
mwenza wa urais wa Chadema iliyokuwa chini ya Umoja wa Katiba ya
Wananchi (Ukawa).
Vyama vingine vinavyounda Ukawa ni NLD na NCCR Mageuzi.
Tangu
kuisha kwa Uchaguzi Mkuu na mgombea wa Chadema kushika nafasi ya pili,
Duni amekuwa kimya, lakini juzi alisema itakapofika Januari mwakani
ataeleza mustakabali wake kisiasa.
“Kwa sasa sisemi
jambo lolote, nitakuambia baadaye kidogo kama nitarudi CUF au nitabakia
Chadema. Kuna mambo ninafanya kwanza, nisingependa kusema,” alisema
Duni.
Pia, Duni alizungumzia hisia zake za kisiasa
visiwani Zanzibar, akisema anashangazwa na kauli ya aliyekuwa Jaji Mkuu
na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Mark Bomani kumshawishi Maalim
Seif Hamad akubali uchaguzi urudiwe.
Siku chache zilizopita, Jaji Boman alinukuliwa na vyombo
vya habari akimtaka Maalim Seif ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais
wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kukubali kurudia uchaguzi huo kama
ilivyotangazwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha
Salum Jecha kuwa utarudiwa ndani ya siku 90.
Jecha
alifuta matokeo ya urais na uwakilishi wa Zanzibar, akisema kulikuwa na
ukiukwaji wa sheria na kanuni na kwamba ndani ya tume yake wajumbe
walitofautiana hadi kukunjana.
Jaji Bomani alisema kama Maalim Seif alishinda, atashinda uchaguzi ukirudiwa kwani wananchi watampigia kura.
Hata
hivyo, Duni alisema: “Anajua kabisa nchi yoyote inaporudia uchaguzi
mara nyingi amani huwa inapotea, kwa mfano Burundi leo hii bado wanauana
na hakuna anayezungumza lolote kwa sababu ni chama tawala kimeshinda.
“CUF
inasisitiza Katiba ya Zanzibar ilindwe au kwa sababu upande wa Bara
wamepata Rais (John Magufuli), sasa hawajali usalama wa Wazanzibari?”
Duni
alihamia Chadema chini ya mpango maalumu wa Ukawa wa kuwezesha vyama
hivyo kuchukua urais Bara na Visiwani, mpango ambao haukuweza kuzaa
matunda.
No comments:
Post a Comment