LIGI KUU ENGLAND Usiku huu imemalizia Raundi ya Mechi zake za 17 kuelekea zile Mechi mfululizo za mwishoni mwa Mwaka kwa mtanange uliochezwa Emirates Jijini London wa Timu ambazo hasa ndizo zinapewa nafasi za kutwaa Ubingwa kwa Arsenal kuifunga Manchester City Bao 2-1.
Ushindi huu umewabakisha Arsenal Nafasi ya Pili wakiwa Pointi 2 nyuma ya Vinara Leicester City wakati City wakiwa Nafasi ya 3 Pointi 4 nyuma ya Arsenal wakifuatiwa na Spurs na Man United ambazo ziko Pointi 3 nyuma huku kila Timu ikiwa imecheza Mechi 17.
Arsenal walitangulia kufunga katika Dakika ya 33 baada ya pasi ya Mesut Ozil kumkuta Theo Walcott Winga ya kushoto na kisha kumhadaa Fulbeki wa City, Bacary Sagna, na kuachia kigongo cha Mguu wa kushoto kilichomshinda Kipa Joe Hart na kutinga.
Dakika ya 45 Olivier Giroud aliipa Bao la Pili Arsenal baada ya kutengenezewa na Mesut Ozil
Hadi Haftaimu Arsenal 2 Man City 0.
Dakika ya 82 City walirudi kwenye Gemu na kuwa 2-1 kwa Goli la Yaya Toure kufuatia kupasiana vyema na yeye kumalizia vizuri kwa shuti la kupinda lililomhadaa Kipa Petr Cesc.
Kuanzia hapo City walikuja juu lakini Arsenal walisimama imara kulinda uongozi wao na kuibuka Washindi.
No comments:
Post a Comment