Monday, 21 December 2015

Hiki ndio kilichofanya Mo Music kupandishwa Mahakamani Dodoma jana

2015 umekuwa mwaka mzuri kwa wasanii wengi underground kufanya vizuri sana, kwenye list  kubwa ya wasanii hao anaingia pia mkali kutoka Mwanza, Mo Music ambaye kadondosha single nyingi zilizomfungulia njia vizuri kwenye game ya muziki.
Kuna kitu kimeendelea upande wa pili na leo December 21 2015 Mo Music amepandishwa Mahakamani Dodoma leo, kuna tatizo ??!!
Kitu ambacho sitoweza kukisahau kwa mwaka 2015 ni mambo ya kesi, sikuwahi kupata kesi tangu nizaliwe… imenipa wakati mgumu sana“- Mo Music.
Kesi yake ilikuwaje >>> “Niliwahi kuwa na uhusiano na msichana mmoja nikaachana nae miezi nane iliyopita… baadae akawa na uhusiano na mtu mwingine, sikujua kuhusu uhusiano wao lakini nikasikia kwamba alikuwa kama anamtapeli huyo jamaa… yule jamaa akahisi yule msichana anachukua pesa na kuleta kwangu. baadae nikapigiwa simu kwamba nina kesi ya kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu. Nikapelekwa Dodoma na kesi iko Mahakamani.”

Maneno mengine ya Mo Music haya hapa kuhusu kesi yake >>> “Kipindi naachia wimbo ‘NITAZOEA’ alisema ana ujauzito wangu, baadae nimeachiwa wimbo wa SKENDO kazusha mengine tena… kesi iko Mahakamani bado
Kesi ya Mo Music imesomwa jana na imeahirishwa mpaka January 13 2016 Mahakama ya Wilaya Dodoma.

No comments:

Post a Comment