Mahusiano ni muhimu sana kwa
kila binadamu hapa duniani na yana mchango mkubwa kwa ufanisi wakila tunalo
lifanya. Kama tuna kubaliana na maelezo hayo basi nilazima kuna umuhimu wa kuya
boresha na kuya imalisha kwani kwa kuto fanya hivyo tuna weza ambulia maumivu.
Zifuatazo ni njia 6 za namna
ya kuboresha kuboresha upendo na mahusiano
1. Kucheka Pamoja na mpenzi wako
Kicheko Ni Mlango Wa Ukaribu, Kama
Mwaweza Kucheka Pamoja Basi Mwaweza Kulia Pamoja, Na Hapa Mwaweza Kuaminiana
Zaidi Katika Kuwasiliana Hisia Zenu, Kama Waweza Kuitofuta Furaha Katika Kila
Kitu Basi Unaweza Kupenya Katika Vyote. Usiwe Mgumu Na Mwenye Msimamo Mkali
Katika Kila Kitu. Jifunze Kujizuia Pale Unapoanza Kuelekea Kwenye Kukasirika Na
Badala Yake Tumia Kucheka Kama Mlango Wa Kutokea. Kama Utaanza Kujizoeza Hivi
Ukiwa Nyumbani, Taratibu Utaweza Ukiwa Ofisini Na Hata Kwingine Kokote.
2. Kutiana Moyo na mpenzi wako
Kila Mmoja Awe Msaada Na Tegemeo Kwa
Mwenzake. Jifunze Kumtia Moyo Na Kumwezesha Mwenzako. Sikiliza Na Kufuatilia
Vile Mwenzako Afanyavyo Au Apendavyo.
Onyesha Heshima Katika Vitu Hivyo
Pia. Kila Upatapo Nafasi Mpongeze Mbele Za Watu Au Hata Unapokua Nae Peke Yenu.
Mjenge Mwenzako Mbele Ya wengine Na Kubali Pongezi Zote Za Mafanikio Yenu
Zimwendee Yeye. Mruhusu Mpenzi Wako Ajue Kuwa Una Mkubali Katika Kila Afanyalo.
Zaidi Tunavyo Wainua Wapenzi Wetu Ndivyo Wanavyotuthamini Na Kutunyanyua Na
Sisi Pia.
3. Kupenda Kugusana na mpenzi wako
Nguvu Ya Mguso Wa Ukaribu Kamwe
Haiwezi Kulinganishwa Na Chochote. Lazima Mjifunze Kujenga Tabia Ya Kugusana
Mara Mpatapo Nafasi Sio Tu Mnapokuwa Mmelala. Kugusana Huku Ni Pamoja Na
Kushikana Mkono Mkiongea Au Mkitembea, Kukumbatia Bega, Kugusa Au Kuchezea
Nyewele Za Mwenzako Na Njia Nyingine Zozote Za Kuonyesha Ukaribu Kimwili. Wengi
Wetu Huweza Kufanya Haya Kidogo Tunapokuwa Peke Yetu Na Kamwe Sio Mbele Ya
Watu, Je, Ni Aibu, Nidhamu Mbaya? Dhambi?
Kugusana Ndiyo Mwanzo Wa Kuamsha Hisia Za Kuhitajiana, (Hebu Jiulize Kisirisiri, Lini Uligusana Na Mwenzako Nje Ya Chumba?). Kumgusa Umpendaye Hukuzuia Kutowaza Kumgusa Yeyote Katika Ulimwengu Uliojaa Wengi Walio Wapweke.
Kugusana Ndiyo Mwanzo Wa Kuamsha Hisia Za Kuhitajiana, (Hebu Jiulize Kisirisiri, Lini Uligusana Na Mwenzako Nje Ya Chumba?). Kumgusa Umpendaye Hukuzuia Kutowaza Kumgusa Yeyote Katika Ulimwengu Uliojaa Wengi Walio Wapweke.
Mguso Huu Wa Upendo Haumaanishi
Mguso Wa Tendo La Ndoa, Ingawa Pia Ni Vyema Kujifunza Kuijenga Lugha Ya Mguso
Wa Tendo La Ndoa Katika Uhusiano Wenu.
4. Zungumza Hisia Zako na za mpenzi wako
Kati Ya Vikwazo Vikubwa Katika
Ustawi Wa Uhusiano Mengi Hususan Ya Wanandoa Ni Kutokuwepo Kwa Majadiliano.
Lazima Wapenzi Wajifunze Kuzungumza Kuhusu Hisia Zao. Kama Vile Maisha Yasivyo
Na Ukamilifu, Uhusiano Na Hata Ndoa Pia Hazina Ukamilifu. Mpenzi Wako Hayuko
Kamili Na Wala Wewe Pia Siyo Mkamilifu. Jifunze Kuzungumza Na Umpendaye Jinsi
Unavyojisikia Na Nini Kinachokusumbua. Kuendelea Na Migogoro Isiyosuluhishwa
Husababisha Moyo Kuwa Baridi Juu Ya Mwenzako. Jiwekeeni Muda Kila Wiki Wa
Kutoka Ili Kuzungumza Mambo Yenu. Mwambie Umpendaye Yapi Yanayojiri Kila Siku
Na Zipi Ni Changamoto Zako Mkiweza Kujifunza Kuwekeza Katika Muda Wa Kuwa
Pamoja Taratibu Hata Muda Wenu Wa Maongezi Ya Simu Utaongezeka.
5. Msamehe mpenzi wako Na Kubali Kusamehewa naye
Kamwe Tusiache Maumivu Na Machungu
Yatawale Uhusiano Wetu. Lazima Tujifunze Kuwasamehe Tuwapendao Na Kujisamehe
Sisi Pia. Kutofautiana Katika Uhusiano Kupo Sana, Na Lazima Tuwape Tuwapendao
Nafasi Ya Kuelezea Vile Vinavyowaudhi Dhidi Yetu. Kila Hisia Za Mmoja Wetu Zina
Umuhimu. Huwezi Kujiona Vile Ulivyo, Mruhusu Mwenzako Akwambie Yanayomuumiza Na
Msameheane.
6. Linda Mwonekano Wa Mpenzi Wako
Mara Nyingi Hatari Hii Hutokea
Tunapokuwa Katika Mizunguko Ya Huku Na Huko. Ukaribu Na Mpenzi Wako
Hauendelezwi Tu Bali Unalindwa. Mwonekano Wetu Lazima Uwe Halisi Na Siyo Bandia
. Vile Tunavyoviona Katika Tamthiliya Na Filamu Siyo Ukaribu Ulio Halisi. Kama
Tunataka Tuonekane Sawa Na Vile Tunavyowaona Wengine Wanavyopendana Basi
Tunakosea Na Kujizuia Kuwa Na Mtazamo Bora Katika Uhusiano Wetu. Ukianza Kupata
Ukaribu Wa Kweli Baina Yako Na Mwenzako, Utapoteza Hisia Ya Kuhitaji Ukaribu
Huo Na Mwingine Yeyote, Na Badala Yake Utaanza Kuulinda Ukaribu Mlionao.
Lengo Liwe Kuvitafuta Vile Vyote
Mpenzi Wako Alivyonavyo Ambavyo Ni Kukuza Ukaribu Wenu. Mwenzako Awe Ndiyo Mtu
Wa Muhimu Kuliko Wote Katika Maisha Yako.
No comments:
Post a Comment