mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Iringa, bi Jesca Msambatavangu amesema
anashangazwa na watu wanaomtuhumu kukihujumu chama hicho wakati wa Uchaguzi
Mkuu Jimbo la Iringa Mjini kwani madai yao hayana uhusiano wowote na sababu za
msingi zilizotumiwa kufungua kesi ya kupinga matokeo ya jimbo hilo,
hivikaribuni.
Akizungumza
na wanahabari ofisini kwake juzi ikuwa ni siku tatu tu baada ya yeye na wajumbe
wengine wa kamati ya siasa ya mkoa akiwemo na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina
Masenza wafungiwe ofisini kwa zaidi ya saa mbili, Msambatavangu alisema:
Alitoa
ufafanuzi huo baada ya kumaliza kikao na baadhi ya vijana wa chama hicho
walioahidi kuendelea kuwa watiifu kwake pamoja na uwepo wa shinikizo kutoka kwa
wanachama wengine wanaoataka ajiuzulu kwa tuhuma za kutungwa.
Pamoja
na kutoa ahadi hiyo ya utiifu, vijana hao walioongozwa na Mwenyekiti wa UVCCM
Manispaa ya Iringa, Kaunda Mwaipyana waliahidi kumpa ulinzi mwenyekiti huyo wa
mkoa katika kipindi anachoendelea na wadhifa wake huo.
Akifafanua
kuhusu tuhuma hizo, Msambatavangu alisema kama madai yanayotolewa dhidi yake
yanaamini na baadhi ya wanaCCM wenzake; kesi iliyofunguliwa na aliyekuwa
mgombea ubunge wa jimbo hilo kupitia chama hicho, Frederick Mwakalebelakwa
vyovyote vile itapoteza uhalali.
pia aliongeza jkua tofauti na majimbo mengine ya mkoa wa Iringa, Iringa Mjini walijipanga vizuri
kushinda uchaguzi huo kwa kuwa walikuwa na rasilimali fedha na watu ya kutosha,
magari, pikipiki na vifaa vingine vingi vya kampeni.
“Badala
ya watu kujiuliza jinsi rasilimali hizo zilivyotumika katika uchaguzi huo, watu
wanazungumzia porojo zinazotungwa dhidi yangu na viongozi wenzangu ambao
nilitofautiana nao mara tu baada ya kuonesha nia ya kutaka kuwania ubunge
katika jimbo la Iringa Mjini, kabla ya kura za maoni za CCM,” alisema.
Alisema
kura za maoni Jimbo la Iringa Mjini zilikuwa na ulaghai mkubwa kwani baadhi ya wanachama
halali wa CCM wakiwemo wale wa muda mrefu walizuiliwa kupiga kura baada ya
majina yao kwa makusudi kutoingizwa kwenye daftari la orodha ya wanachama.
Aliwataka
wanahabari kupita katika kata mbalimbali za jimbo hilo ili kujionea ukweli huo
ambao kwa kiasi fulani uliwakasirisha wana CCM ambao leo wakilaumiwa kwa
matokeo ya uchaguzi jimbo hilo itakuwa ni sawa na kutowatendea haki.
“Iringa
Manispaa lazima tujipange upya, tujifunze kuweka watu wanaokubalika na wananchi,
sio wanaokubalika na viongozi. Watu walidhani wanapambana na mimi, kumbe
wanapambana na wanachama wa mkoa mzima kwasababu wao ndio walioniamini wakanipa
madaraka haya niliyonayo ambayo wengine hawataki niendelee kuwa nayo,” alisema.
Akizungumzia
tukio la vijana wenzake kuifungia kamati ya siasa ya mkoa wa Iringa ofisini,
Mwenyekiti wa UVCCM Manispaa ya Iringa, Kaunda Mwaipyana alisema kilichofanywa
na vijana hao hakikubaliki na ni kinyume na kanuni za umoja huo.
“Kesho
nitakuwa na kamati ya utekelezaji, tutapitia kanuni zetu ili tuone namna tutakavyowawajibisha
vijana wote waliohusika katika tukio lile,” alisema.
Mbali
na Mkuu wa Mkoa wa Iringa na Msambatavangu, wengine waliokutwa na kadhia ya
kufungiwa ofisini na vijana hao ni pamoja na Kaimu Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa
Elisha Mwampashi na Katibu Mwenezi wa Mkoa Dk Yahaya Msigwa.
Wengine
ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa
Ephraim Mhekwa, Godfrey Mosha, aliyekuwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,
Mahamudu Mgimwa ambaye pia ni Mbunge wa Mufindi Kaskazini na aliyekuwa Mwenyekiti
wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo, Joseph Muhumba.
Mwaipyana alisema moja ya jukumu kubwa la UVCCM kwa chama hicho ni kulinda usalama wa
viongozi wake na sio kufanya kile kilichofanywa na vijana hao hata kama wana
malalamiko kwani wanapaswa kuzingatia katiba, kanuni na taratibu ili wanachokilalamikia
kifanyiwe kazi.
No comments:
Post a Comment