Monday, 21 December 2015

JE? UNGEPENDA KUIJUA HII STORY KUTOKA HUKO CHINA SOMA MWENYEWE UJIONEE...

Mgahawa mmoja nchini China umepatikana ukitoza wateja wake gharama ya ''kupumua hewa safi ''.Mgahawa huo ulioko Mashariki mwa China, katika mji wa Zhangjiagang , mkoa wa Jiangsu unatoza wateja wake Yuan moja sawa na centi za dola ($0.15; ) kwa kusafisha hewa safi ndani ya mgahwa huo.
Yamkini pesa hizo ni zinatumika kuendesha kiyoyozi na mashine mengine ya kusafisha hewa shirika la habari la China Xinhua limeripoti.
Miji mingi nchini China zimeghubikwa na ukungu mkubwa unaotokana na mabadiliko ya tabia nchi yanayochochewa na hewa mkaa inayotoka viwandani.
Katika miji mingi nchini humo ni vigumu kuona umbali wa mita 100 kutokana na ukungu mzito uliosababisha serikali kuagiza viwanda vifungwe kwa siku kadhaa juma lililopita.



Kwa sasa watu wanashauriwa wavalie barakoa ilikupunguza madhara ya hewa chafu.
Mmiliki wa mgahawa huo alinunua mashine ya kusafisha hewa na akalazimika kuongeza bei ya vyakula ilikufidia gharama yake.
Hata hivyo hakufwata kanuni zinazosimamaia bei ya vyakula wala hakutoa ilani kwa wateja wake.
Maafisa wa mji huo walimlazimisha kufutilia mbali gharama hiyo wakisema hawezi kuwauzia wateja wake ''hewa safi'' shirika la kitaifa la Xinhua linasema.

Hata hivyo masharti makali ya idara ya manispaa ya mji huu yaliwakasirisha sana baadhi ya wateja wa mgahawa huo, ambao wanasema kuwa ni haki yao kupumua hewa safi.
''Kwa hakika ni wajibu wa Manispaa kuhakikisha mazingira ni masafi lakini sasa wameshindwa kutekeleza wajibu wao na wanamuadhibu mtu ambaye amejitahidi kuhakikisha wateja wake wanapumua hewa safi ''anasema mteja mmoja kupitia kwa mtandao wa Sina Weibo.

No comments:

Post a Comment