Saturday, 26 December 2015

ARSENAL WASHIDWA KUONGOZA LIGI BAADA YA KUKUBALI KIPIGO KUTOKA KWA SOUTHAMPTON....

Image result for southampton vs arsenal
Arsenal wameikosa nafasi murua ya kuongoza Ligi Kuu England walipotandikwa Bao 4-0 huko kwa Uwanjani kwa Mtakatifu Maria walipobamizwa Bao 4-0 na Southampton maarufu kama Watakatifu.
Magoli ya Southampton yalianza kwa Bao la Fulbeki Cuco Martina, akianza Mechi yake ya kwanza kabisa ya Ligi, kwa Shuti la Mita 30 na Bao hilo kudumu hadi Haftaimu.
Kipindi cha Pili, Southampton walipiga Bao nyingine 3 katika Dakika za 55, 69 na 90 kupitia Shane Long, Jose Fonte na Shane Long tena.
Matokeo haya yamewaacha Arsenal wakiwa Nafasi ya Pili wakiwa Pointi 2 nyuma ya Vinara Leicester City ambao nao Jana walichapwa 1-0 na Liverpool.
Nako huko Saint James Park, Bao pekee la Dakika ya 90 la Kiungo Tom Cleverly limewapa ushindi wa Bao 1-0 Everton walipocheza na Wenyeji wao Newcastle.




No comments:

Post a Comment