Thursday, 5 November 2015

VIWANGO VYA UBORA VILIVYO TOLEWA NA FIFA TANZANIA UGANDA ZAPANDA

6, NOVEMBER 2015

Kenya na Tanzania zimepanda kwenye orodha mpya ya viwango vya soka duniani iliyotolewa leo na shirikisho linalosimamia soka duniani, Fifa.
 
 Kenya imepanda hatua sita hadi nambari 125, nayo Tanzania ikapanda hatua moja na kutua nambari 135. Taifa Stars walisonga kwenye mechi za kufuzu kwa Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi kwa ushindi wa jumla wa 2-1 dhidi ya Malawi. Malawi wamo nambari 97 kwenye orodha hiyo.

Ivory Coast ndiyo inayoongoza barani Afrika katika nambari 22, ikifuatwa na Algeria iliyo nambari 26 nayo Ghana nambari 30.

Uganda ndio walio mbele miongoni mwa mataifa ya Afrika Mashariki, wakikwamilia nambari 68 baada ya kupanda hatua saba.

Rwanda wamo nambari 96 baada ya kushuka hatua tatu nao Burundi nambari 107 baada ya kupanda hatua sita.

Congo Brazzaville wamo namba 52, wakifuatwa kwa karibu na DR Congo walio nambari 55.
Sudan wameshuka hatua 44 hadi nambari 128, na Ethiopia hatua sita hadi 117.

Sudan Kusini waliocheza mechi yao ya kwanza ya kufuzu kwa Kombe la Dunia dhidi ya Mauritania, ambayo walitoka sare 1-1 lakini wakabanduliwa kwenye marudiano baada ya kucharazwa 4-0, wanashikilia nambari 134 baada ya kupanda hatua 10.

Djibouti ndio wanaoshika mkia Afrika wakiwa nambari 207, wakifuatwa na Somalia nambari 203 na Eritrea 202.

Duniani, orodha ya timu kumi bora ndiyo hii:

1 Ubelgiji
2 Ujerumani
3 Argentina
4 Ureno
5 Chile
6 Uhispania
7 Colombia
8 Brazil
9 Uingereza
10 Austria

No comments:

Post a Comment