Thursday, 5 November 2015

UNAJUA WAZIRI WA UINGEREZA AMESISITIZA NINI KUHUSU USAFIRI WA NDEGE

 6,NOVEMBER 2015

  

Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron amesema kwamba anaweka usalama wa raia wa Uingereza kwanza katika uamuzi ya kusitisha safari za ndege katika rasi ya Misri ya Sharm el-Sheikh.


Akisimama pembeni ya Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi ,baada ya mazungumzo baina yao mjini London,bwana Cameron amesema nchi hizo mbili zinashirikiana kwa karibu zaidi katika suala la usalama,baada ya ajali ya ndege mali ya shirika la ndege la Urusi ililyoanguka nchini Misri mwishoni mwa wiki iliyopita na kuua abiria wote waliokuwa ndani ya ndege hiyo.

Cameron ametilia mkazo kuhusu imani yake kuwa ndege hiyo huenda ilidunguliwa kwa bomu.
Rais Sisi amesema kwamba Misri imeweka utaratibu wa ziada wa ukaguzi katika Rasi ya Sharm miezi kumi iliyopita kutokana na ombi lililotolewa na Uingereza.

Shirika la ndege la ujerumani na Uholanzi Lufthansa nazo zimesitisha safari kuingia Misri.

No comments:

Post a Comment