Tuesday, 17 November 2015

MIKOPO YA AWAMU YA NNE KWA WANAFUNZI ELIMU YA JUU


Image result for HESLB logo tanzania

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inapenda kuwafahamisha waombaji wa mikopo kwa mwaka wa masomo 2015/2016 kuwa imetoa orodha ya AWAMU YA NNE yenye jumla ya waombaji wa mwaka wa kwanza 718 waliopangiwa mikopo.
Itakumbukwa kuwa wiki iliyopita, Bodi ilitoa orodha ya Awamu ya Tatu iliyokuwa na waombaji 6,915 waliopangiwa mikopo. Kati ya waombaji hao waliopangiwa mikopo, waombaji 4,642 ni walikua ni wale wanaojiunga na shahada ya kwanza katika vyuo mbalimbali nchini na waombaji 2,273 ni wanafunzi wanaojiunga na Stashahada (Diploma) ya Ualimu wa masomo ya sayansi na hisabati katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).
Kwa msingi huo, Bodi inapenda kuufahamisha umma kuwa hadi sasa imekwishawapangia mikopo jumla ya waombaji mikopo wenye sifa 48,469 wa mwaka wa kwanza. Katika awamu ya kwanza, Bodi ilitoa orodha yenye jumla ya waombaji12,282; Awamu ya Pili wanafunzi 28,554; Awamu ya Tatu wanafunzi 6,915 na Awamu hii ya Nne wanafunzi 718wamepangiwa mikopo.
Majina yote ya waombaji waliofanikiwa kupangiwa mikopo kutoka katika awamu zote tatu yanapatikana kupitia mtandao wa Bodi wa www.olas.heslb.go.tz na tovuti ya Bodi ambayo ni www.heslb.go.tz Aidha, orodha hizo pia zimetumwa vyuoni kwa ajili ya taratibu za usajili 




No comments:

Post a Comment