Thursday, 12 November 2015

MAREKANI YAIONDOLEA LIBERIA VIKWAZO

 Image result for obama's image

 Marekani imeiondolea Liberia vikwazo vya kiuchumi huku Ras Barack Obama akiipongeza nchi hiyo kwa kujitolea kufanikisha demokrasia tangu kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe 2003.
Vikwazo hivyo viliwekwa miaka 11 iliyopita dhidi ya kiongozi wa wakati huo Charles Talyor ambaye kwa sasa yumo gerezani kwa makosa ya uhalifu wa kivita.
Kwa mujibu wa ikulu ya White House, Rais Obama amesema hali kwamba utawala wa Taylor ulimalizika na yumo gerezani ina maana kwamba vikwazo hivyo havihitajiki.
Alisema sasa yeye na washirika wake hawana uwezo wa kuhujumu ufanisi wa Liberia.
Msemaji wa baraza la usalama wa taifa Marekani Ned Price amesema Marekani inataka kuwapongeza watu wa Liberia “kwa kujitolea kwao kudumisha amani na demokrasia” ambako kumewezesha kuondolewa kwa vikwazo hivyo.
Taylor na washirika wake waliendeleza vita katili vya wenyewe kwa wenyewe 1991-2002 nchini Liberia vilivyosababisha vifo vya maelfu ya watu.
Alikamatwa 2006 na kushtakiwa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu mjini Hague na makosa 11 ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu kwa makosa yaliyotekelezwa na waasi aliowasaidia katika taifa jirani la Sierra Leone.

No comments:

Post a Comment