Wednesday, 18 November 2015

KOMBE LA DUNIA 2018; ECUADOR YAPAA JUU, ARGENTINA YAJIVUTA, BRAZIL YAPANDA

Ecuador wameendelea kukaa kileleni mwa Kanda ya Marekani ya Kusini ya kuwania kucheza Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 huko Russia huku Argentina wakiambua ushindi wao wa kwanza na Brazil kupaa hadi Nafasi ya 3 baada kupata ushindi mnono.

Ecuador, wakicheza Ugenini, waliichapa Venezuela Bao 3-1 kwa Bao za Fidel Martinez, Jefferson Montero na Felipe Calcedo wakati Bao la Vezuela likifungwa na Josef Martinez.
Nao Argentina wameambua ushindi wao wa kwanza waliposhinda Ugenini kwa kuifunga Colombia 1-0 kwa Bao la Lucas Biglia la Dakika ya 20.

Brazil, wakicheza kwao huko Arena Fonte Nova, waliifunga Peru Bao 3-0 kwa Bao za Douglas Costa, Renato Agusto na Filipe Luis.

Wakiwa Nyumbani, Uruguay waliitandika Chile 3-0 na Wafungaji walikuwa Diego Godin, Maximiliano Pereira na Jose Martin Caceres.


KOMBE LA DUNIA 2018
Marekani ya Kusini-Mechi za Mchujo
Ratiba/Matokeo:
**Saa za Bongo
Alhamisi Novemba 12
Bolivia 4 Venezuela 2
Ijumaa Novemba 13
Ecuador 2 Uruguay 1
Argentina v Brazil [Mechi imeahirishwa kutokana na Mvua]
Chile 1 Colombia 1
Jumamosi Novemba 14
Argentina 1 Brazil 1
Peru 1 Paraguay 0
Jumanne Novemba 17
Colombia 0 Argentina 1
Jumatano Novemba 18
Venezuela 1 Ecuador 3
Paraguay 2 Bolivia 1
Uruguay 3 Chile 0
Brazil 3 Peru 0
++++++++++++++++++++++
KOMBE LA DUNIA 2018
Marekani ya Kusini-Mechi za Mchujo
MATOKEO
Alhamisi Oktoba 8
Bolivia 0 Uruguay 2
Colombia 2 Peru 0
Venezuela 0 Paraguay 1
Chile 2 Brazil 0
Argentina 0 Ecuador 2
Jumatano Oktoba 14
Ecuador 2 Bolivia 0
Uruguay 3 Colombia 0
Brazil 2 Venezuela 0
Paraguay 0 Argentina 0
Peru 3 Chile 4

No comments:

Post a Comment