Friday, 30 October 2015

Full Time ya Man City Vs Crystal Palace na matokeo ya mechi nyingine za Capital One October 28 (+Pichaz&Video)




Kama ambavyo usiku wa October 27 michezo kadhaa ya Kombe la Capital One iliendelea na tulishuhudia Chelsea wakitolewa kwa mikwaju ya penati 5-4 dhidi ya Stoke  City mara baada ya kumaliza dakika 120 kwa sare ya goli 1-1. Usiku wa October 28 ilichezwa michezo minne ya Capital One.
man-city-palace-bony
Miongoni mwa mchezo uliyochezwa usiku wa October 28 ni mechi kati ya Manchester City dhidi ya Crystal Palace, mchezo ambao ulichezwa katika dimba la Etihad, Man City wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani wamefanikiwa kuibuka na ushindi mnono wa jumla ya goli 5-1.
Generated by IJG JPEG Library
Magoli ya Man City yalifungwa na Wilfried Bony dakika ya 22, Kevin de Bruyne dakika ya 44, Kelechi Iheanacho dakika ya 59 kabla ya Yaya Toure kupachika goli la nne kwa mkwaju wa penati dakika ya 76 wakati Crystal Palace wakihangaika kupata goli la kufutia machozi na kufanikiwa kufunga dakika ya 89 kupitia kwa Damien Delaney, Man City dakika moja baadae wakaongeza goli la tano kupitia kwa Manu Garcia.
man-city-palace-iheancho_1
Matokeo ya mechi nyingine za Capital One October 28
  • Liverpool 1 – 0 AFC Bournemouth
  • Southampton 2 – 1 Aston Villa
  • Manchester United 0 – 0 Middlesbrough ( Mikwaju ya penati Man United 1-3 Middlesbrough)
image

No comments:

Post a Comment