Uwanja wa Nangwanda Sijaona umeendelea kuwa mgumu kwa Yanga baada ya
kushindwa kupata ushindi kwa mara nyingine kufuatia kulazimishwa suluhu
na Ndanda kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania.
Mchezo wao wa kwanza dhidi ya Ndanda kwenye uwanja wa Nangwanda,
Yanga walichezea kipigo cha goli 1-0 ikiwa ni mchezo wa kwanza kwa
Ndanda kucheza dhidi ya Yanga ntangu walivyopanda daraja.
Mshambuliaji
wa Yanga Obrey amecheza kwa mara ya kwanza mechi ya ligi kuu ya Vodacom
Tanzania bara wakati Yanga ikicheza dhidi ya Ndanda FC kwenye uwanja wa
Nangwanda Sijaona, MtwaraGolikipa
wa Ndanda FC Jeremia Kisubi alikuwa akipoteza muda kwenye mchezo dhidi
ya Yanga na kupelekea mwamuzi kutoa adhabu ya mkwaju wa adhabu ndogo
ndani ya eneo la 18 baada ya kipa huyo kudaka mpira na kukaa nao kwa
muda
Matokeo hayo yameendelea kuzifanya timu hizo huongeza idadi ya
michezo waliyotoka sare. Ndanda na Yanga zimeshakutana mara 5 hadi sasa,
Yanga imeshinda mechi moja sawa na Ndanda ambayo nayo imeshinda mechi
moja huku timu hizo zikiwa zimetoka sare michezo mitatu.
Donald Ngoma (kushoto) akiwania mpira na beki wa Ndanda FC
Ndanda ikiwa inacheza mchezo wake wa kwanza kwenye uwanja wa nyumbani
iliweza kuhimili mashambulizi ya Yanga ambayo pia ilikuwa ikicheza
mchezo wake wa kwanza ugenini tangu kuanza kwa ligi msimu wa 2016-2017.
Licha ya kufanya mashambulizi ya mara kwa mara, wachezaji wa Yanga
walishindwa kupata goli na kujikuta wakipata kona nyingi kutokana na
walinzi wa Ndanda kuokoa mashambulizi ya hatari yaliyofanywa na Yanga.
SalumTelela
amecheza mechi yake ya kwanza dhidi ya imu yake ya zamani (Yanga) ikiwa
ni baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa misimu sita mfululizo
No comments:
Post a Comment