Wednesday, 3 August 2016

Asubiri mpenziwe siku 10 katika uwanja wa ndege

Asubiri mpenziwe siku 10 katika uwanja wa ndege

Je penzi la kweli lipo ?
Hilo ndilo swali linaloulizwa sana katika mitandao nchini China.
Hii ni baada ya raia mmoja kutoka Uholanzi kusafiri maelfu ya kilomita ili kukutana na mpenziwe raia wa uchina ambaye walikutana kwenye mitandao ya kijamii.

Hata hivyo mpenziwe hakujitokeza hata baada ya kusubiri katika uwanja wa ndege kwa siku 10!
Amini usiamini alimsubiri kwa siku 10!
Alexander Pieter Cirk, 41, alifunga safari hadi jimbo la Hunan kukutana na mpenziwe mwanamke kutoka Uchina ambaye anafahamika kwa jina Zhang.
bi Zhang mwenye umri wa miaka 26 anasema alidhania kuwa ulikuwa ni mzaha tu
Na baada ya kumsubiri kwa siku kumi katika uwanja wa ndege wa Changsha hakujitokeza ,,Cirk alienda kufanya subira na mwishowe akalazimika kulazwa hospitalini kwa uchovu wa mwili na roho.
Cirk ameviambia vyombo vya habari kuwa walikutana na bi Zhang mwenye umri wa miaka 26 miezi miwili iliyopita na penzi lao likachipuka.
Hata hivyo alipofika China akagundua kuwa wanawake wengi nchini humo wanafanana, na akashindwa kumpata Zhang kwa simu.
Ripoti hiyo ilipopeperushwa kwenye runinga ya taifa , bi Zhang alijitokeza na kuwaamnbia Wachina kuwa alidhania kuwa ni utani tu kama vile maisha ya mjini kwa wanawake wengi ambao huambiwa kuwa wanapendwa.
''Ni kweli kuwa tulikuwa tunapendana lakini nilianza kumshuku huenda alikuwa ananichezea shere''
Alinitumia picha za tiketi ya ndege na hakunipigia simu baada ya hapo''
Kwa hivyo nikapuuza nikijua kuwa ni mzaha tu''bi Zhang aliiambia Hunan TV.
Alexander Pieter Cirk alilazwa hospitalini baada ya kuzimia
Zhang alisema kuwa ule wakati alipokuwa akimtarajia ,yeye alikuwa amefanyiwa upasuaji katika mji mwengine wa mbali.
Hangeweza kumpokea katika uwanja wa ndege.
katika mitandao ya kijamii tukio hilo limewaacha wengi wasijue iwapo ilikuwa ni penzi la kweli ama ni ujinga wa kuzaliwa.

No comments:

Post a Comment