Manchester United kwa sasa ipo China
kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu na mashindano
mbalimbali, kama ilivyo kawaida kwa mashabiki wa soka wanapokutana na
wachezaji au makocha wao huwa wanaomba wasainiwe vitabu vyao vya
kumbukumbu au jezi.
July 22 2016 kocha wa Man United Jose Mourinho ameingia kwenye headlines baada ya kugoma kusaini jezi ya Chelsea aliyoombwa na shabiki wakati akiendelea kusaini jezi za mashabiki wa Man United, Mourinho wakati anasaini alionekana kuikwepa jezi ya Chelsea huku akitikisa kichwa kuashiria kugoma.
No comments:
Post a Comment