Msanii
maarufu wa Vichekesho (Komedi) kutoka kundi la Vituko Show Ndugu.
Ismail Issa Makombe a.k.a KUNDAMBANDA, amefariki dunia usiku wa kuamkia
leo.
Kundambanda
alikuwa mgombea ubunge wa CUF na UKAWA kwenye jimbo la Masasi - Mtwara
katika uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi Disemba 2015 baada ya ule wa
Oktoba kutofanyika kutokana na kifo cha aliyekuwa mgombea wa awali wa
UKAWA, Mhe. Emmanuel Makaidi (NLD).
Katika
uchaguzi huo wa Disemba 2015 Kundambanda alipata kura 14,069 dhidi ya
kura 16,597 za (mshindi) Rashid Chua Chua kutoka CCM. Taratibu za
mazishi zinafanyikia nyumbani kwao Masasi.
No comments:
Post a Comment