Rais wa
Simba Sport Club Evans Aveva akizungumza na Vyombo vya Habari leo
wakati wa Uzinduzi wa Simba Week Akiwa Sambamba Katibu Mkuu wa Simba
Patrik Kahemela (Kulia) na Afisa Masoko na Mawasiliano Kutoka Eaggroup
Richard Ryaganda( kushoto) .
Simba
inasherehekea wiki maalum iliyo Batizwa Jina la Simba Week
ambayoImezinduliwa Leo na Rais wa Simba Sport Club Ndugu Evans Aveva na
hufikia kilele chake Tarehe 8 Mwezi Agosti. Mwaka huu siku hii ya Simba
week itakuwa na uzito wa kipekee kwani Klabu ya Simba itakuwa inaanza
Sherehe za kuadhimisha Miaka 80 ya klabu Hiyo. Sherehe za Wiki ya Simba
zinaenda sambamba na dhima yetu ya kuendeleza Mabadiliko chanya ndani ya
Simba bado inaendelea kushika kasi, Katika kipindi cha mwaka mzima.
Katika
Kipindi Hiki Simba Sport Club imekuwa na utaratibu wa kuwa na siku
maalum kwaajili ya kufurahi, kuwatambulisha Rasmi wachezaji,Jezi za timu
na kujiandaa kwa Msimu Mpya, siku hii imekuwa Maarufu kama Simba Day.
Tangu Ianzishwe imekua ikiboreka Siku hadi siku, mwaka huu Imeona ni
Muhimu kuiboresha zaidi na hususani kuangalia Mchango wa timu Hiyo kwa
Jamii inayoizunguka.
Simba iliamua kuanzisha Simba Week ambayo lengo lake kuu ni kuwa wiki ya Simba Sports Club kufanya kazi za Jamii, kukuza vipaji vya soka vya vijana, kutembelea Wadau wa Maendeleo na pia Shughuli Nyingine Zenye Tija kwa Timu..Siku ya Simba Day, Simba Sports Club itacheza Mechi naInter Clube ya Angola kwenye Mechi hii Wachezaji Wapya wataonekana Rasmi baada ya Maandalizi.
No comments:
Post a Comment