Rais wa
Marekani Barack Obama amemsifu sana mgombea wa chama cha Democratic
Hillary Clinton na kusema ndiye afaaye zaidi kuongoza Marekani.
Akihutubu
katika kongamano kuu la chama cha Democratic mjini Philadelphia, huku
akishangiliwa na wajumbe, Rais Obama amesema hakujawahi kuwa na mtu
aliyehitimu zaidi kuongoza Marekani kuliko Bi Clinton.
"Hakujawahi
kuwa na mwanamume au mwanamke, iwe mimi au Bill Clinton au mtu mwingine
yeyote aliyekuwa amehitimu zaidi kuwa rais kama yeye," amesema Bw
Obama.
Amemsifu
pia kwa kujikakamua na kuwa mwanamke wa kwanza katika historia ya taifa
hilo kuteuliwa kuwa mgombea urais wa chama kikubwa.
Obama ameshutumu sera za Donald Trump
Amempongeza kwa kubomoa vizuizi na kuunda nafasi zaidi kwa Wamarekani.
Amewaahidi Wamarekani kwamba Bi Clinton anatetea umoja na maadili ya Wamarekani.
Bw Obama pia amemkosoa vikali mgombea wa chama cha Republican Donald Trump.
Awali, Seneta wa Virginia Tim Kaine alikubali rais uteuzi wa kuwa mgombea mwenza wa Bi Clinton. BBC
No comments:
Post a Comment