Aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida na baadaye kuhama chama na kujiunga na CHADEMA, Mgana Msindai ametangaza kurudi CCM.
Msindai
alitangaza uamuzi huo jana mjini Dodoma baada ya kupewa nafasi na
Mwenyekiti Mstaafu wa CCM, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete wakati anaendesha
mkutano mkuu wa CCM uliomchagua Rais Dk John Magufuli kuongoza chama.
Msindai
alisema aliamua kurudi CCM baada ya kuona kuwa sasa hakuna cha kupinga
baada ya Rais Magufuli kuchaguliwa kuwa rais wa nchi.
Msindai
aliingia CHADEMA baada ya aliyekuwa mgombea wa Ukawa, Edward Lowassa
kujiunga na Chadema mwaka jana wakati wa uchaguzi mkuu.
No comments:
Post a Comment