Thursday, 30 June 2016

SIRI IMEFICHUKA? MAN UNITED WAANIKA PICHA JEZI YA JINA LA HENRIKH MKHITARYAN KWENYE TOVUTI YAO!


MANUNITED-MKHITARYAN-JEZIManchester United hii Leo inaonekana wamekurupuka kuweka Jezi zao za Mechi za Ugenini kwenye Tovuti yao huku zikiwa na Jina la Henrikh Mkhitaryan.
Mkhitaryan, mwenye Miaka 27, ameripotiwa kuhamia Man United baada ya Ofa yao ya Pauni Milioni 26.3 kukubaliwa na Klabu ya Germany Borussia Dortmund huku pia ikiaminika kuwa Mchezaji huyo ameshaafiki maslahi yake binafsi na kilichobaki ni kupimwa afya yake.
Lakini kabla ya mambo yote kuwa rasmi na kukamilika kwa Dili kutangazwa, Picha za Jezi zikaibuka kwenye Tovuti ya Man United zikitangaza Jezi zao za Mechi za Ugenini za Msimu ujao zikiwa na Jina Mkhitaryan Mgongoni.
Picha za Jezi hizo hazikudumu muda mrefu kwebye Tovuti hiyo kwani baadae Leo zikatolewa.
Hata hivyo, Dili ya Man United kumchukua Mkhitaryan bado iko pale pale na inatarajiwa kukamilika muda wowote kuanzia sasa na kumfanya awe Mchezaji wa Pili kununuliwa chini ya Meneja Mpya Jose Mourinho baada ya Wiki iliyopita kumnasa Eric Bailly kutoka Villareal.

No comments:

Post a Comment