Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
ameyaagiza mashirika yote ya Hifadhi ya jamii kutoendelea kuwekeza
katika miradi ya majengo na badala yake yajielekeze katika ujenzi wa
viwanda na miradi mingine inayozalisha ajira na kuchangia zaidi katika
pato Ia taifa.
Rais Magufuli ametoa maelekezo hayo leo Jumatatu tarehe 09 Mei, 2016
alipofungua majengo mawill ya vitega uchumi ya Mfuko wa Pensheni (PPF)
na Shirika Ia Hifadhi ya Jamii(NSSF) yaliyopo Jijini Arusha.
Pamoja na kuyapongeza mashirika hayo kwa kujenga majengo ya kisasa
jijini Arusha na maeneo mengine hapa nchini, Dkt. Magufuli amekosoa
uwekezaji mkubwa unaofanywa na mashirika hayo kwa kujenga majengo ya
gharama kubwa ambayo licha ya kuwa wananchi wa kawaida hawawezi kumudu
gharama za kupanga kwa ajlli ya kuendesha shughull zao, hayana manufaa
ya kutosha ikilinganishwa na endapo mashirika hayo yangewekeza katika
miradi inayozalisha ajira nyingi, faida ya haraka na kuchangia kwa kiasi
kikubwa katika palo Ia taifa.
"Hii mifuko ya hifadhi ya jamii kuanzia leo muache kuwekeza katika
majengo, wekezeni kwenye viwanda, leo mngekuwa na viwanda vya sukari
hawa watu wasingetuchezea kuficha sukari, na inawezekana hata kama
ingepungua tungewambia nyinyi agizeni sukari.
"Mchango wa mifuko ya hifadhi za jamii katika nchi yetu, ambayo iko
saba, imekuwa ikichangia pato la taifa kwa asilimia 12, lakini hifadhi
ya jamii sehemu nyingine duniani, imekuwa ikichangia palo la taifa kwa
asilimia 40, kwa hiyo kuna mahali tumekosea, na ndio maana mlipokuwa
mkizungumza hapa sijui mlijua nitakayowaambia, ninawapongeza mliwekeza
katika majengo, jengo Ia PPF na jengo IB NSSF ukipiga hesabu za kawaida
haya majengo yamegharimu zaidi ya shilingi bllioni 60, lakini tujiulize
hawa wananchl waliosimama hapa watayatumiaje haya majengo" Amesema Dk.
Magufuli huku akishangiliwa na wananchi wa Arusha waliojtokeza
kushuhudia ufunguzi huo.
No comments:
Post a Comment