Kijana mmoja wa
mjini Mumbai ambaye amekuwa akiugua ugonjwa usio kawaida wa jeni ambao
huufanya mwili kuzeeka mara nane zaidi ya ilivyo kawaida amefariki.
Nihal Bitla mwenye umri wa miaka 15 alikuwa mwanaharakati wa India anayefanya kampeni dhidi ya ugonjwa huo kwa jina Progeria.Bitla aligonga vichwa vya habari alipokuwa akitafuta wagonjwa wengine 60 wanaougua ugonjwa huo ili kushiriki katika yake mjini Boston.Alianzisha mtandao wa kijamii kutoa hamasa kuhusu ugonjwa huo.
Hivi karibuni alianzisha hamasa kwa jina #HatsOnProgeria,ambapo alionekana na kundi moja la wafuasi wake katika kituo cha reli cha Chhatrapati Shivaji.
Bitla alipata umaarufu baada ya kukutana na nyota wa Bollywood Aamir Khan mnamo mwezi Disemba baada ya ukurasa wake wa facebook kuzungumzia kuhusu habari yake na swala kwamba alikuwa shabiki mkubwa wa nyota huyo.
Alifariki hospitalini siku ya Jumanne kusini mwa jimbo la Telangana,ambapo alikuwa ameenda kuhudhuria sherehe za harusi.
Ripoti za vyombo habari zinasema kuwa huenda alikosa maji mwilini kutokana na joto katika eneo hilo.
No comments:
Post a Comment