Sunday, 21 February 2016

Wanaume hawapendi aina hizi za wanawake

Ukiachilia mbali uzuri wa mtu, tabia yake utanashati na mengine mengi kila mwanaume ana radha anayoitafuta kwa mwanamke anae mtaka, hii inatofautiana kati ya  mtu na mtu siwezi kuongelea nini mwanaume anatafuta kwa mwanamke, ila najua  wanaume watakuwa wanajua nini kinawavutia kwa mtoto wa kike, ila najua kuna aina Fulani za wanawake wanaume wengi hawapendi kuwa nao.
Waongeaji Sana
Wanawake wa maneno mengi,wanaume  hawapendi mwanamke mlopokaji wanawake wa aina hii huwa hawajui nini waongee na nini wasiongee au wakati gani wa kuongea na wakati gani wa kunyamaza. Watu wa aina hii hawajui kuuliza wao wanafoka tu mwanzo mwisho
Wasiopenda kusema wanachotaka
Kuna baadhi ya wanawake huwa wanahisi wanaume zao wanaoteshwa ndoto juu ya mahitaji yao, hawasemi nini wanataka lakini wasipopatiwa wanalalamika sana, hii inamuwia vigumu mwanaume kumuelewa mwanamke wa aina hii, sababu huwa haweki wazi  hisia zake au mambo ambayo anapenda afanyiwe na mpenzi wake. Bila kujua mwanaume sio malaika
Waliliaji Ndoa
Wapo wanawake wanawaza ndoa kila wakati, na wakati mwingine ni kwa sababu tu wanaona rafiki zao wanaolewa basi kila siku anakuuliza utanioa lini? Aina hii ya wanawake ndo kichefuchefu kwa wanaume walio wengi.
Wabinafsi
Wale wanawake wanaojiweka wao kwanza kwa kila kitu, anajali maisha yake kwanza na familia yake na ndo mwanaume afwate, mwanamke wa aina hii yuko radhi kuomba pesa nyingi kwajiri ya matumizi yake binafsi kuliko kujali mko katika hali gani kiuchumi. Na wepesi kukuacha kama hutimizi mahitaji yake muhimu.
Wanaojiona wako Juu Zaidi
“Much know” aina hii ya wanawake wao wanajua kila kitu, hawa wanaitwa “much know” wanataka kutawala kila kitu,hadi akili ya mwanaume, wanaume wengi hawapendi kuendeshwa na inakuwa vigumu kama upo katika uhusiano na mwanamke wa aina hii na ukadumu. Wanawake wa aina hii hawatofautiani sana na wale  wenye maneno mengi.

No comments:

Post a Comment