Lipsticks ni kama urembo kwa wanawake wengi na wengine wanapaka tu ili wafanane na rangi za nguo zao, wenyewe wanaita matching lakini kuna ukweli nyuma ya rangi hizo na nitajaribu kuchambua rangi mbalimbali ambazo wanapaka watoto wa kike siku hizi.
Haina maana kila mwanamke anajua maana ya rangi hizi za midomo ndo maana wengine wanapaka tu kama fasheni ila pia usianze kuwatazama wasichana midomo yao sababu tu umejua maana hizi au usitumie maana hizi kuwakashifu baadhi ya wasichana.
Nyekundu
Tunajua nyekundu ni hatari au mapenzi, mwanamke anaependa rangi nyekundu huyu yupo tayari kwa lolote au tunaweza sema hawa ndo wale wanaitwa Ready for Action. Wana jiamini na wanasimamia misimamo yako ila inaweza kuwa kwa uzuri au ubaya, inategemeana na mtu. Na kwasababu nyekundu inaonekana sana wanawake wanaopenda kupaka hii pia wanapenda sana kuonekana (attention) lazima akiingia sehemu umuone.
Rangi ya Machungwa(orange)/peach
Wapole, wanataka wanaume watulivu, wanapenda watu wanaowajili, wanaojua kumuheshimu mwanamke, na hawana makeke,
Nyeusi
Wachache wanatumia rangi, hii kwa sababu pia ni moja kati ya rangi inayo shangaza sana ukitumia kama lipstick,ila ukikutana na watu wanaopenda rangi hizi ni zaidi ya machizi, hawa ni watundu hadi kitandani na usipokuwa makini utatolewa knockout.pia ni watu wasiopenda kujichanganya na wengine mara nyingi wanaotumia rangi nyeusi ni kama ishara ya kaa mbali, “keep away” au “leave me alone”
Pinki
Hii rangi ya pekeake inamaanisha “nakupenda siwezi sema” kuwa tayari kumsoma binti anaetumia rangi za pinki mda wote akiwa na wewe, ukute anatamani umpe busu na wewe huelewi, wengine wanaita innocent, japokuwa kuna aina nyingi za rangi ya pinki na zingine zinaweza kuwa na maana tofauti inategemea na mpakaji. Usije ukapata wazo moja tu kwa kutazama maana moja, maana zinaweza kuwa nyingi kutokana na mgawanyo wa rangi kuwa makini na hilo.
Brown
Hawa ni watu wanaojipenda na kijielewa, na rangi hii sio ya kun’gara sana kwahiyo inatumika na watu wanaopenda utulivu, wanawake wasiopenda au tuseme wasiopenda (too much attention) kuonekana sana tofauti na ilivyo kwa wanawake wanaopenda nyekundu,wanawake wa namna hii tunaweza kusema “they keep low profile”
Zambarau
Hii inasimama kama rangi ya kuonyesha uwezo (power), yaani wanawake walio na majukumu na wanajitegemea.
No comments:
Post a Comment