Timu nane zinazoundwa na cdc na mawakala wa maswala ya afya walienda kwenye maeneo yaliyoathirika na kuchukua sampuli ya damu na kuwahoji wamama walioathirika na wamama ambao watoto wao walizaliwa wakiwa na vichwa vidogo.
Katika kipindi cha majuma yajayo, watakusanya taarifa kutoka kwa mamia ya wamama katika jimbo la paraeeba, jimbo la pili lililoathirika zaidi.
Katika Ripoti ya siku ya jumanne Wizara ya Afya ya Brazil imethibitisha watoto 587 wana vichwa vidogo.asilimia 75 zaidi ya wiki iliyopita huku maelfu ya watoto wanachunguzwa.
Baada ya kutangazwa hali ya taadhari ya kiafya, Rais wa Shirika la Afya duniani, Margaret Chan aliwasili Brasilia kufuatilia hali ilivyo.
Akiwa huko alikutana Rais wa Brazil,Dilma Roussef siku ya jumanne na kusema kuwa anafurahishwa na namna Serikali inavyoshughulikia tatizo hilo na kutaka jamii isaidiwe kupambana na mbu anayeeneza virusi vya Zika
No comments:
Post a Comment