RAUNDI YA MTOANO YA TIMU 16
Mechi zote kuanza Saa 4 Dakika 45 Usiku
JUMANNE 16 FEB 2016
Benfica v Zenit Saint Petersburg
Paris St Germaine v Chelsea
KEPTENI JOHN TERRY hayumo kwenye Kikosi cha Chelsea kilichoruka Mchana wa Leo kuelekea Paris, France ambako Kesho Jumanne Usiku watatinga ndani ya Parc des Princes kucheza na Paris Saint-Germain katika Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA CHAMPIONZ LIGI, UCL.
Licha ya Leo Terry kufanya Mazoezi na wenzake Jijini London, Sentahafu hakuwemo kwenye Timu iliyopanda Ndege kwenda Paris kutokana nab ado kusumbuliwa na maumivu ya Musuli za Pajani aliyopata kwenye Mechi ya Ligi Kuu England Jumamosi iliyopita.
Kwenye Mechi hiyo ambayo Chelsea waliibamiza Newcastle 5-1, Terry, mwenye Miaka 35, alitolewa Kipindi cha Kwanza na Nafasi yake kuchukuliwa na Baba Rahman.
Pengo hili linaweza kumfanya Meneja wa Chelsea, Guus Hiddink, kumuanzisha Baba Rahman Fulbeki ya Kushoto na Branislav Ivanovic kuchukua nafasi ya Terry kwenye Sentahafu huku Cesar Azpilicueta akicheza kama Fulbeki wa Kushoto.
DONDOO MUHIMU:
-Hii ni mara ya 3 mfululizo kwa PSG na Chelsea kukutana Raundi za Mtoano za UEFA CHAMPIONZ LIGI.
-Uso kwa Uso:
2015
-11/3/2015: Chelsea 2 PSG 2
-17/2/2015: PSG 1 Chelsea 1
**PSG ilisonga kwa Bao za Ugenini
2014
-8/4/2014: Chelsea 2 PSG 0
-2/4/2014: PSG 3 Chelsea 1
**Chelsea ilisonga kwa Bao la Ugenini
Kikosini yumo Oscar, ambae hakucheza Mechi ya Jumamosi na Newcastle, na pia yupo Mchezaji mpya aliesainiwa Januari, Matt Miazga, pamoja na Chipukizi wa Miaka 18 Jake Clarke-Salter.
Ndani ya Ndege kwenda Paris, pia alikuwemo Kiungo Nemanja Matic licha ya kuwa Kifungoni kwenye Mechi hii na PSG lakini Mbrazil mpya, Alexandre Pato, ameachwa Jijini London.
KIKOSI CHA CHELSEA KILICHOSAFIRI: Thibaut Courtois, Asmir Begovic, Jamal Blackman, Branislav Ivanovic, Baba Rahman, Cesc Fabregas, Oscar, Eden Hazard, John Mikel Obi, Bertrand Traore, Kenedy, Pedro, Loic Remy, Diego Costa, Matt Miazga, Nemanja Matic, Ruben Loftus-Cheek, Willian, Gary Cahill, Cesar Azpilicueta, Jake Clarke-Salter
VIKOSI VINAVYOTARAJIWA:
PSG:
Trapp, Van der Wiel, Thiago Silva, Luiz, Maxwell, Motta, Rabiot, Matuidi, Di Maria, Ibrahimovic, Lucas
Chelsea:
Courtois, Azpilicueta, Ivanovic, Cahill, Baba Rahman, Mikel, Oscar, Pedro, Fabregas, Willian, Costa
REFA: Carlos Velasco Carballo [Spain]
UEFA CHAMPIONZ LIGI
RAUNDI YA MTOANO YA TIMU 16
**Mechi zote kuanza Saa 4 Dakika 45 Usiku isipokuwa inapotajwa
JUMATANO 17 FEB 2016
KAA Gent v VfL Wolfsburg
AS Roma v Real Madrid
JUMANNE 23 FEB 2016
Arsenal v Barcelona
Juventus v Bayern Munich
JUMATANO 24 FEB 2016
Dynamo Kiev v Man City
PSV Eindhoven v Atletico Madrid
Marudiano
JUMANNE 8 MAR 2016
Real Madrid v AS Roma
VfL Wolfsburg v KAA Gent
JUMATANO 9 MAR 2016
2000 Zenit St Petersburg v Benfica
Chelsea v Paris St Germaine
JUMANNE 15 MAR 2016
Atletico Madrid v PSV Eindhoven
Man City v Dynamo Kiev
JUMATANO 16 MAR 2016
Barcelona v Arsenal
Bayern Munich v Juventus
TAREHE MUHIMU:
Raundi za Mtoano:
-Droo ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16: Desemba 14
**Mechi Februari 16/17/23/24 na Marudiano Machi 8/9/15/16
-Droo ya Robo Fainali: Machi 18
**Mechi Aprili 5/6 na Marudiano Aprili 12/13
-Droo ya Nusu Fainali: Aprili 15
**Mechi Aprili 26/27 na Marudiano Mei 3/4
FAINALI
Mei 28
San Siro, Milan, Italy
No comments:
Post a Comment