Takriban watu 140
wameuawa kwa milipuko ya mabomu katika miji ya Homs na Damascus nchini
Syria, waangalizi na vyombo vya habari vya serikali vimeeleza.
Takriban
milipuko minne ilitokea katika eneo la Sayyida Zeinab mjini Damascus na
kuua takriban watu 83. Awali mjini Homs Watu 57 wengi wao raia waliuawa
kwa mashambulizi ya mabomu yaliyokuwa yametegwa kwenye magari mawili.Wanamgambo wa Islamic State wamekiri kutekeleza mashambulizi hayo katika miji hiyo miwili.
Wakati huo huo, Waziri wa mashauri ya kigeni wa Marekani, John Kerry amesema makubaliano ya muda yamefikiwa kati Marekani na Urusi kuhusu suluhu ya mgogoro wa Syria.
No comments:
Post a Comment