SERIKALI
imesema itatoa bei elekezi katika sekta ya afya hivi karibuni baada ya
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kubariki bei hizo kuanza kutumika kwa lengo
la kuwapunguzia mzigo wa gharama wananchi.
Bei
elekezi kwa vituo vya afya zimeshasainiwa na Waziri wa Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na baadhi ya vituo vya afya
vimeshaanza kutumia bei hiyo.
Aidha,
serikali imepanga kuweka utaratibu wa wagonjwa kwenda kutibiwa katika
Hospitali ya Taifa Muhimbili ikiwa ni hatua ya kupunguza msongamano wa
wagonjwa katika hospitali hiyo.
Hayo
yameelezwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto
na Wazee, Dk Hamis Kigwangalla wakati akizungumza na waaandishi wa
habari baada ya kuzindua Matokeo ya Utafiti wa Kutathimini utoaji wa
huduma za afya nchini kwa mwaka 2014/2015.
No comments:
Post a Comment