Tuesday, 23 February 2016

MECHI YA SIMBA NA YANGA YAINGIZA MILIONI 500 KASORO KIDOGO TAIFA


Image result for simba na yanga

MECHI ya mzunguko wa pili ya Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara kati ya watani wa jadi, Yanga na Simba iliyofanyika juzi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam imeingiza zaidi ya Sh. milioni 490.
Taarifa zilizopatikana jana jijini zinaeleza kuwa wenyeji wa mchezo huo Yanga wao walipata mgawo wa Sh. milioni 139 wakati Wekundu wa Msimbazi, Simba waliambulia Sh. milioni 99.

"Mechi imeingiza kama Sh. milioni 490, na taarifa za awali ni kwamba tiketi za Sh. 7,000 na za VIP A zilizokuwa zinauzwa Sh. 30,000 ziliuzwa zote," alisema kiongozi mmoja wa Simba.
Katika mchezo huo, Yanga ambao ni mabingwa watetezi walifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 na kufikisha pointi 46 zilizowafanya pia warejee kileleni kwenye msimamo wa ligi hiyo inayoshirikisha timu 16.
Mabao katika mechi hiyo iliyochezeshwa na refa mwanamke, Jonesia Rukyaa yalifungwa na Donald Ngoma na Amissi Tambwe.

No comments:

Post a Comment