Manchester City wataipa kipaumbele Mechi yao ya Jumanne ya UEFA CHAMPIONZ LIGI, UCL, badala ya ile ya Jumapili ya Raundi ya 5 ya EMIRATES FA CUP dhidi ya Chelsea huko Stamford Bridge kwa mujibu wa Meneja wao Manuel Pellegrini.
City wanacheza Mechi yao ya kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UCL ugenini na Dynamo Kiev hapo Jumatano na Siku 4 baadae wapo Wembley kucheza Fainali ya Capital One Cup na Liverpool.
Pellegrini, Raia wa Chile, ameeleza: “Kupaumbele ni Mechi inayofuata lakini kwa sababu ya majeruhi safari hii ni ile ya Jumanne.”
City wanakabiliwa na Mechi za Mashindano Manne ndani ya Siku 11 kuanzia Februari 21 hadi Machi 2.
City – Mechi zao za Mashindano Manne ndani ya Siku 11:
-Jumapili Februari 21: Chelsea FA Cup huko London
-Jumatano Februari 24: Dynamo Kiev UCL huko Kiev
-Jumapili Februari 28: Liverpool Fainali C1C huko London
-Jumatano Machi 2: Liverpool Ligi Kuu England huko Anfield
Pellegrini aliongeza: "Tuna Wachezaji 13 tu wanaoweza kucheza Jumapili na Jumatano tunacheza UEFA CHAMPIONZ LIGI. Tutaangalia nani wanaweza kucheza.”
Chelsea, ambao wako Nafasi ya 12 kwenye Ligi Kuu England, walicheza Mechi yao ya UCL Jumanne iliyopita na kufungwa 2-1 na Paris Saint-Germain huko Paris.
Meneja wa Chelsea, Guus Hiddink, ambae alitwaa FA Cup alipokuwa na Chelsea kwa mara ya kwanza Mwaka 2009, amesema: "Tuna Mechi kali ya FA Cup!"
EMIRATES FA CUP
Raundi ya 5
Jumamosi Februari 20
1545 Arsenal v Hull City
1800 Reading v West Brom
1800 Watford v Leeds
2015 Bournemouth v Everton
Jumapili Februari 21
1700 Blackburn v West Ham
1800 Tottenham v Crystal Palace
1900 Chelsea v Man City
Jumatatu Februari 22
2245 Shrewsbury v Man United
THE EMIRATES FA CUP 2015/16
TAREHE MUHIMU
Raundi ya 3
Ijumaa 9 Januari 2016
Raundi ya 4
Jumamosi 30 Januari 2016
Raundi ya 5
Jumamosi 20 Februari 2016
Raundi ya 6-Robo Fainali
Jumamosi 12 Machi 2016
Nusu Fainali
Jumamosi 23 Aprili 2016 & Jumapili 24 Aprili 2016
Fainali
Jumamosi 21 Mei 2016
No comments:
Post a Comment