Sunday, 21 February 2016

CHELSEA WAIBAMIZA MAN CITY 5 - 1 KOMBE LA AF CUP

 

FA CUP
Matokeo:
Raundi ya 5
Jumapili Februari 21
Blackburn 1 West Ham 5   
Tottenham 0 Crystal Palace 1      
Chelsea 5 Man City 1



West Ham, Crystal Palace na Chelsea Leo zimeweza kutinga Robo Fainali ya EMIRATES FA CUP kwa kishindo baada ya kupata ushindi mnono.
West Ham na Crystal Palace zote zilishinda Ugenini kwa West Ham kuishindilia Blackburn Rovers Bao 5-1 na Crystal Palace kuitungua Tottenham 1-0.
Katika Mechi ya mwisho hii Leo, Chelsea, ikicheza kwao Stamford Bridge, iliibamiza Man City, iliyochezesha Kikosi dhaifu, Bao 5-1.
Bao za Chelsea zilifungwa na Diego Costa, Dakika ya 35, Willian, 48, Gary Cahill, 53, Eden Hazard, 67, na Traore, 89, wakati lile la City lilifungwa Dakika ya 37 na David Faupala.
VIKOSI:
Chelsea (Mfumo 4-2-3-1): Courtois; Azpilicueta, Cahill, Ivanovic, Baba Rahman; Fabregas, Mikel; Pedro, Willian, Hazard; Diego Costa.
Akiba: Begovic, Miazga, Matic, Loftus-Cheek, Oscar, Traore, Remy.
Manchester City (Mfumo 4-4-2): Caballero; Zabaleta, Adarabioyo, Demichelis, Kolarov; M Garcia, Fernando, A.Garcia, Celina; Iheanacho, Faupala.
Akiba: Hart, Clichy, Humphreys, Kompany, Fernandinho, Barker, Sterling.
REFA: Andre Marriner
EMIRATES FA CUP
Raundi ya 5
Jumatatu Februari 22
2245 Shrewsbury v Man United   
THE EMIRATES FA CUP 2015/16
TAREHE MUHIMU
Raundi ya 3
Ijumaa 9 Januari 2016
Raundi ya 4
Jumamosi 30 Januari 2016
Raundi ya 5
Jumamosi 20 Februari 2016
Raundi ya 6-Robo Fainali
Jumamosi 12 Machi 2016
Nusu Fainali
Jumamosi 23 Aprili 2016 & Jumapili 24 Aprili 2016
Fainali
Jumamosi 21 Mei 2016

No comments:

Post a Comment