23,2,2016
OFISI
ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imeokoa Sh
bilioni 4.38 ambazo zingetumika na watumishi wa Halmashauri mbalimbali
nchini kwa ajili ya safari za ndani.
Waziri
wa Tamisemi, George Simbachawene alibainisha hayo katika kipindi
maalumu cha Siku 100 za Serikali ya Awamu ya Tano kinachorushwa na kituo
cha televisheni cha TBC1 cha Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).
“Katika
kipindi cha siku 95, tumeweza kuokoa kiasi kikubwa cha fedha ambazo
watumishi wa halmashauri wangezitumia katika safari za ndani zisizo na
tija na hazijalenga kumkomboa mwananchi huyu ambaye hana dawa na hana
barabara,” alisema Simbachawene.
Akizungumzia
uwajibikaji wa watumishi katika halmashauri nchini, Simbachawene
alisema ili kuhakikisha halmashauri hizo zinafanya kazi ipasavyo,
wameunda kitengo cha ukaguzi ambacho kina kazi ya kudhibiti na
kufuatilia utendaji wa kazi za halmashauri.
“Tamisemi
tuna deni kubwa, kwani sisi ndio tunaotegemewa na wizara kutafsiri
mipango yao ya elimu afya, miundombinu na sekta nyingine. Tamisemi ni
wakala wa serikali kwa wananchi,” alisema na kuongeza kuwa watendaji
wa halmashauri ambao hawataki kwenda na kasi ya Rais Magufuli, basi
wataondolewa katika nafasi zao bila kuonewa haya.
“Tutahakikisha
tunawachukulia hatua wezi wote, wabadhirifu na wasio waadilifu, huwezi
utupishe. Tutawapima kwa jinsi wanavyoondoa kero kwa wananchi,”
alisema na kukiri kuwa katika halmashauri kuna matatizo ya uadilifu
jambo linalofanya miradi mingi kushindwa kukamilika na ikikamilika
inakuwa chini ya kiwango.
Aidha, amewataka wakurugenzi kuhakikisha wanawafikia wananchi na kumaliza kero za wananchi kinyume chake kazi wataiona chungu.
Kuhusu
ukusanyaji wa mapato, Simbachawene alisema asilimia 95 ya halmashauri
zote zimeanza kutumia mfumo wa elektroniki katika kukusanya mapato na
kuwa zile chache ambazo hazijaanza zimetakiwa kufanya hivyo baada ya
kuongezewa muda kidogo.
No comments:
Post a Comment