Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi
limepitisha bajeti ya zaidi ya Shilingi bilioni 67.6 Katika kikao maalum
cha baraza la Madiwani kwa mwaka 2016/2017 ikiwa ni makisio ya
mwaka mpya wa fedha utakaoanza mwezi Julai mwaka
huu.
Makisio ya bajeti hiyo yamegawanyika katika sehemu kuu tatu, ambazo makusanyo ya ndani yanayokadiriwa kufikia kiasi cha jumla ya Shilingi bilioni 4,189,145,436 , ruzuku kutoka serikali kuu zaidi ya shilingi bilioni 44.063 ambazo ni kwa ajili ya mishahara na matumizi ya kawaida, huku miradi ya maendeleo ikiwa na jumla ya shilingi 21,294,808,400
Akiizungumzia bajeti hiyo, Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Bi. SAADA MALUNDE, amebainisha kuwa, Halmashauri imeanzisha vyanzo vipya vya mapato ambapo kuanzia mwaka wa Fedha 2016/2017 Halmashauri inatarajia kuanza kutoza kodi za majengo kwa wakazi wake pamoja na tozo ya ushuru wa madini kwa kuzingatia vigezo vitakavyowekwa kwa lengo la kuongeza mapato ya ndani.
Akizungumza wakati akifunga kikao cha baraza hilo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi FESTO MGINA, ametoa rai kwa Madiwani na wataalam wa Halmashauri ya Mufindi kuhakikisha kwa pamoja, wanashirikiana katika suala la ukusanyaji wa mapato mara baada ya kuanza kwa mwaka mpya wa Fedha ili Halmashauri iweze kufikia malengo na kutoa huduma kwa jamii.
Aidha, Mgina ametanabaisha kuwa, pamoja na randama ya bajeti hiyo kwa mwaka ujao wa Fedha, Halmashauri imeambatanisha maombi maalum kwa serikali kuu ambayo ni pamoja ombi la shilingi Shilingi milioni 550,000,000 kwa ajili ya ukarati wa shule ya Malangali ikiwa ni miongoni mwa shule kongwe hapa nchini ambazo viongozi wengi wa Taifa hili walipata kusoma.

No comments:
Post a Comment