Wednesday, 20 January 2016

MAN CITY: YAYA TOURE KUTIMKA, BONY AKANA KUTAKA KUONDOKA

Image result for yaya toureKIUNGO wa Manchester City Yaya Touré anatafakari kuihama Klabu hiyo mwishoni mwa Msimu huu kwa mujibu wa Wakala wake, Dimitri Seluk.
Mkataba wa Toure, mwenye Miaka 32, na City unamalizika Mwakani Mwezi Juni na awali Mchezaji huyo wa Ivory Coast alisikika akisema atabaki City lakini Wiki hii zimeibuka Ripoti kuwa Klabu ya China, Shanghai SIPG, inataka kumsaini.
Seluk amekiri kuwa wao wapo tayari kusikiliza Ofa yeyote.
Akiongea na Jarida la SportItalia, Seluk alieleza: “Hatahama Januari. Lakini mwishoni mwa Msimu mambo yanaweza kubadilika. Tupo tayari kusikiliza Ofa yeyote ile.”
Wakati huo huo, Mchezaji mwenzake Toure wa City na Ivory Coast, Wilfried Bony, amekanusha uvumi kuwa anataka kuihama City.
Imedaiwa Bony anataka kurudi Klabu yake ya zamani Swansea City baada ya kumhoji Meneja Manuel Pellegrini kwanini hakumuanzisha kwenye Mechi na Arsenal Mwezi Desemba.
LIGI KUU ENGLAND
Ratiba
**Saa za Bongo            
Jumamosi 23 Januari 2016
1545 Norwich v Liverpool           
[Mechi kuanza Saa 12 Jioni]
Crystal Palace v Tottenham                  
Leicester v Stoke             
Man United v Southampton                  
Sunderland v Bournemouth                  
Watford v Newcastle                  
West Brom v Aston Villa             
2030 West Ham v Man City                  
Jumapili 24 Januari 2016
1630 Everton v Swansea            
1900 Arsenal v Chelsea 

No comments:

Post a Comment