wabunge wa Uingereza wazozana mjadala wa kuivamia IS
Wabunge nchini
Uingereza wamegombana katika mjadala kuhusu mpango wa serikali kujiunga
katika harakati za pamoja za kijeshi zinazoongozwa na Marekani kupambana
na wanamgambo wa Islamic State ndani ya Syria.
Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron amelitaja kundi hilo kama tishio kubwa kwa usalama wa taifa.
Cameron amesema kuwa mashambulizi dhidi ya kundi hilo yataisaidia Uingereza kuwa salama. Hata hivyo Kiongozi wa upinzani , Jeremy Corbyn, amesema mabomu ya Uingereza yataua raia wasio na hatia.Amesema
wananchi wa Syria wangetaka mzozo huo kutatuliwa kwa njia ya amani na
kwamba ana hamu ya kuona wakimbizi wa Syria waliopiga kambi barani Ulaya
wakirejea nyumbani.
Baada ya mjadala, wabunge watapiga kura kuidhinisha au kupinga mpango huo.
Waziri
wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry amesifia juhudi za David Cameron
na kuelezea matumaini kuwa wabunge wataidhinisha mpango huo. wali Cameron alishurutishwa kuomba radhi kwa
wabunge baada ya kusema wale wanaopinga mashambulizi makali dhidi ya
Islamic state wanaiunga mkono kundi hilo.Baada ya mjadala huu wa saa 10 wabunge wataamua iwapo majeshi ya Uingereza yatajiunga na Ufaransa Marekani na Urusi.
No comments:
Post a Comment