Kocha Garry Neville ameanza na ‘mkosi’ baada ya mechi yake ya kwanza akiwa benchi kuishuhudia Valencia ikitandikwa nyumbani kwa mabao 2-0 na Lyon.
Sasa kikosi cha Neville kinakwenda kukutana na timu
yake ya zamani ya Manchester United ambayo jana iliporomoka huko.
Neville anaifundisha Valencia akiwa anasaidiwa na
mdogo wake, Phil Neville na wote waliowahi kuichezea Manchester United kwa
mafanikio makubwa.
H. BABA AIBUKA NA WIMBO
WA RHUMBA
A+
A-
Print
Email
MWANAMUZIKI wa Kizazi Kipya ‘Bongofleva’, Hamisi Ramadhani ‘H Baba’, ni
kama ameamua kubadili staili yake ya muziki kwa sasa kwa kutoka na wimbo
mpya wenye mahadhi ya Rhumba.
H. Baba anayetambulika kwa staili yake ya cheza kwa ufasaha, sasa
ameamua kutoka kivingine kabisa tofauti na mashabiki wake walivyomzoea.
Akiongea na Saluti5, H. Baba alisema ni mapema mno kutaja jina la wimbo
wake huo mpya anaotarajia kuuachia mwishoni mwa mwezi huu, kwani anataka
uwe ‘surprise’ ya mwaka kwa mashabiki wake.
“Kuna baadhi ya wasanii wana tabia ya kuiba kazi za wenziwao, hivyo
wimbo huu sitautaja jina hadi hapo nitakapokuwa tayari kuuachia,”
alisema H. Baba.
H. Baba alisema wimbo huo wenye staili hiyo mpya iliyochanganyika na
vionjo vya muziki kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC),
ameurekodia C9 Records iliyo chini ya C9 Kanjenje.
Soma zaidi hapa >>: http://www.saluti5.com/2015/12/h-baba-aibuka-na-wimbo-wa-rhumba.html
Copyright © saluti5
Soma zaidi hapa >>: http://www.saluti5.com/2015/12/h-baba-aibuka-na-wimbo-wa-rhumba.html
Copyright © saluti5
HOMA YA MAFUA YAMTESA
MARIAH CAREY
A+
A-
Print
Email
MWANAMUZIKI Mariah Carey wa Marekani alilazimika kukimbizwa hospitalini
mjini New York, Jumatano iliyopita kutokana na kubanwa na mafua makali.
Alilazimika kupatiwa matibabu yanayoambatana na vifaa vya kumtia joto,
vitamin pamoja na dawa za kupambana na vidudu vinavyosababisha homa kali
na kushindwa kupumua.
Kuna uwezekano mkubwa homa hiyo ikampunguzia ratiba yake ya maonesho
ambapo Jumamosi iliyopita angetumbuiza New Jersey.
Soma zaidi hapa >>: http://www.saluti5.com/2015/12/homa-ya-mafua-yamtesa-mariah-carey.html
Copyright © saluti5
Soma zaidi hapa >>: http://www.saluti5.com/2015/12/homa-ya-mafua-yamtesa-mariah-carey.html
Copyright © saluti5
MWANAMUZIKI Mariah
Carey wa Marekani alilazimika kukimbizwa hospitalini mjini New York,
Jumatano iliyopita kutokana na kubanwa na mafua makali.
Alilazimika kupatiwa matibabu yanayoambatana na vifaa vya kumtia joto,
vitamin pamoja na dawa za kupambana na vidudu vinavyosababisha homa kali
na kushindwa kupumua.
Kuna uwezekano mkubwa homa hiyo ikampunguzia ratiba yake ya maonesho
ambapo Jumamosi iliyopita angetumbuiza New Jersey.
Soma zaidi hapa >>: http://www.saluti5.com/2015/12/homa-ya-mafua-yamtesa-mariah-carey.html
Copyright © saluti5
Soma zaidi hapa >>: http://www.saluti5.com/2015/12/homa-ya-mafua-yamtesa-mariah-carey.html
Copyright © saluti5

No comments:
Post a Comment